USIPENDE KULETA MAZOEA KWENYE MAHUSIANO:


Ukweli ni kwamba watu wengi tunaishi kwa mazoea kwenye mahusiano na ndoa zetu, Tunawachukulia poa wenza wetu ndo maana mambo yana haribika. Mwenza wako anapoona unamchukulia poapoa, unamdharau kamwe hawezi
kufurahia. Lazima mtakasirikiana, mtatukanana na hata kupigana

Ni muhimu sana wapendanao kuwa na mipaka ya kimazungumzo, Kujielewa kwamba unazungumza na mwenza wako utumie lugha gani. Sio unazungumza na mwenza wako kama vile unazungumza na marafiki zako, jaribu kubadilika kidogo. Kuwa na heshima na mwenza wako sababu huyo ndio mtakayetengeneza "taasisi yenu ya muda mrefu, Unaachaje kumheshimu mwenza wako ambaye ndiye unayelala naye, ndiye ambaye una mipango naye na ndiye mtakayekuwa pamoja kwa miaka mingi zaidi pengine kuliko hata wazazi wako.? .

Huyo ndiye msiri wako wa maisha. Nazungumza hili kwa sababu kwa kawaida mara nyingi huwa wapendanao wanakutana ukubwani, kila mtu anakuwa ametoka kwenye misingi yake Kila mmoja anakuwa amelelewa katika malezi tofauti hivyo msipokuwa makini kusomana tabia, hakika hamuwezi kufika mbali,.

Yawezekana mwenza wako akawa na tabia fulani ambayo si nzuri lakini kwa kuwa ndio umemchagua, unapaswa kumuongoza taratibu ili aweze kubadilika, Kujishusha kuna faida pale kunapotokea malumbano, msitoe nafasi ya kutawaliwa na hasira hapo hakika mtadumu.

Whatsapp 0629241898
#Saikolojiatz

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA