WANAUME WENGI WAMEJIKUTA KATIKA LAANA YA NDOA ZAO BILA WAO KUJUA KWANI WALISHIKILIA MAISHA YA MWANAMKE ASIYE NA HATIA





Ahadi ya ndoa ni agano la MUNGU kwa wana wa adamu, Mtu mke na Mtu mume kuingia makubaliano ya kuilinda AHADI YA NDOA kama ambavyo wataapa mbele ya MAHEKARU YA IBADA. 
Kwa sasa wanaume wengi wanaingia kwenye ndoa kuwafurahisha wanawake ili warahisishe matakwa yao kwa wanawake, huku wakitumia nyumba za ibada katika kuhalalisha uongo wao, muda mwingine unakutana na Mwanamke anasema;- 
👉 BILA NDOA HUJAGUSA MWILI WANGU. 
Wakati huo TAMAA imechukuwa nafasi yake ndipo pilika za NDOA zinaanza ili tu kutafuta kutimiza lengo, bila kujua kwamba;- 
👉 NDOA NI KIFUNGO CHA MAPENZI📍 Yawezekana Mwanaume anajua atawezaje kujinasua katika kifungo hicho ila ugumu upo kwa Mwanamke ambaye yeye anaamini katika AGANO LA NDOA.
Kumiliki maisha ya mwanamke huku ukijua huna malengo nae ni kujiweka katika LAANA japo wengi hawajui.
Usizuie maisha ya Mwanamke huku ukijua huna malengo nae, huo ni utekaji ambao mbinu zake ni kutumia MAPENZI wakati huo huo tabia za wanaume akiisha pata penzi ni rahisi kumzoea Mwanamke na ndipo tatizo huanzia kiasi cha kumfanya Mwanamke kukosa tumaini katika mapenzi🤔
Wakati Mwanamke akiendelea kuumia na kukosa FURAHA NA AMANI hapo ndipo Mwamuzi wa kweli "MUNGU" huinuka kutafuta mkosaji ili ahukumu, Japo wakati huo Mwanaume atakuwa busy kujifurahisha na Wanawake wengine🤦‍♂️
Epuka kupata LAANA ya Mwanamke kupitia NDOA ni hatari kwa maisha yako Mwanaume.
#Elista_kasema_ila_sio_Sheria 

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA