LINDA MVUTO WAKO AMBAO MWENZA WAKO ALISHAWISHIKA NAO ILI USIJE MFANYA AKAONA HUMVUTII TENA






Kumekuwa na tabia ya mazoea dhidi ya wana MAHUSIANO NA NDOA ukiangalia unakuta ni hali ya kuona mwenza wake hana jipya tena📍
Mvuto wako ndiyo uliotengeneza hitaji lake kwako, kama utapoteza mvuto huo tarajia kuwa wa kawaida kwake😂
Mapenzi yanalindwa na MVUTO na huo ndiyo unajenga HAMU dhidi yako kinyume chake huna maana tena, Katika hali isiyokuwa ya kawaida wengi wanapo ingia Kwenye MAHUSIANO/NDOA wanaacha kulinda MIVUTO yao kisa tu tayari wamepata walicho kihitaji, Mtu Kabla ya kupewa nafasi ama kutoa nafasi alikuwa katika kujenga ushawishi kwa Mwenza wake, aliweza kuwa msafi na nadhifu lakini alipo ingia Kwenye Mahusiano ama ndoa hakujali kulinda mvuto wake🤔
Wengine kabla ya kupewa nafasi waliwekeza MUDA wao pamoja na kutoa ZAWADI ambazo hizo ndio zilijenga tumaini la UPENDO 💘
Kuna wengine kabla ya kutoa nafasi walikuwa wanaajituma katika kuhakikisha Mtu anafurahia penzi, lakini baadaye mambo hayako kama yalivyo tazamiwa💔
Kama ile hali ya MVUTO iliyoweza kuwa sababu ya udhaifu wa mwingine ikidumu basi WEWE UTABAKIA KUWA WA THAMANI KWAKE na kama ikitoweka basi ujue kubakia kwake kwako ni huruma yake, na Muda wowote anaweza kuondoka ili kulinda UTASHI wake, Kwa sababu UTASHI huzaliwa na MVUTO wa mwingine💯

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA