ACHA KABISA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO KWENYE MAPENZI

Kumlilia mtu ambae kule aliko ana furahi na mtu mwingine kabisa na hata jina lako yawezekana ameshalisahau.




Kukakata tamaa ya kuingia ktk Ndoa kisa tu kila mwanamke au mwanaume uliye mpata hakuonyesha nia kuishi nawe. Wapo wengi na bora zaidi yako na hawajakata tamaa vuta subira tu muda muafaka upo!




Kujidhalilisha au kujidharau kisa kipato chako kidogo sio vizuri ,ongeza juhudi upate zaidi tena kile kilicho halali. Ili mradi unaishi wewe ni tajiri wa baadae ukiamsha ndoto zako.




Kumchukia mtu aliye kusababishia maumivu na matatizo iwe ndugu,rafiki au mpenzi. Badala yake usisahau ulicho jifunza kwa alicho kufanyia ili usirudie makosa.




Kujipendekeza kwa mwanaume au mwanamke ambae anakuona wa kawaida,. Yaani mawasiliano yenu mpaka umuanze wewe. Akikuanza yeye basi ujue ana shida na ngono au pesa.
Achana na mtu wa hivyo ni kichomi.







Yenye kuridhishana kwa pande zote na sio kumridhisha yeye tu, huo ni ubinafsi katika mahusiano na yanakondesha na kuua.







fanya subra na kusali tumehusiwa
hilo namuomba Allah atupe sote
wenza wenye kher nasi kwa wakati
sahihi na watu sahihi Thuma Ammyn



Muu Mata