DALILI KWAMBA MTOTO WAKO ANANYANYASWA KINGONO!
(1) Anakua na ndoto za usiku za mara kwa mara, za kutisha, kuogopa, unakuta usiku anapiga kelele mara kwa mara na kukosa usingizi kusikoeleweka.
(2) Aanakua na mawazo au ukiwa naye anakua hayupo kabisa, mfano wenzake wanacheza yeye akili yake uonaona haip kwenye mchezo, amejikalia pembeni kajikunyata, wenzake wananagalia TV, wanakula lakini unaona kichwa chake hakipo kabisa wakati mwingine mpaka umshitue.
(3) Ghafla ulaji wake una baddilika, alikua anakula vizuri ila hali tena anakataa, anakosa hamu ya kula na anapata shida katika kumeza chakula, achana na wale watoto tangu wachanga ni wagumu kula, yeye ni ghafla hali.
(4) Ghafla anabadilika, anakua ni mtu wa kukasirika kasirika, anakua na gasira zile za ghafla anaweza hata kupiga wenzake, anakua muoga muoga, hajiamini na si mtu wa kujichanganya kabisa, anakua mtu wa peke yake peke yake.
(5) Stori zake zinabadilika, anaku mtu wa kuongelea mapenzi, anachora chora kwenye madaftari au kuandika mambo ambayo yanaashiria mapenzi.
(6) Anaanza kuwa msiri na mambo yake, haongei tena mamboa ambayo labda anafanya shuleni, kwenye basi na siri nyingine kama hizo.
(7) Amepata rafiki mpoya shuleni au mtaani, anamzungumzia huyop rafiki kila wakatio, mara flani hivi, flan kanipa zawadi na mambo kama hayo.
(8) Anaanza kuwa na tabia za kikubwa, kuanzia kuongea, kuonyesha tabia za kufanya mapenzi, akicheza na wenzake kuwafanyisha mapenzi na anajua mambo mengi ya kikubwa.
(9) Ghafla ana pesa, ana vizawadi zawadi vipya ambavyo hata hujui kama vinatoka wapi, anakua na vitu vingi ambavyo havieleweki.
(10) Anaanza kuona aibu, hataki tena kuvua nguo mbele za wakubwa, labda Mama yake, bado mdogo lakini kama hataki kuogeshwa na kuguswa mwili wake.
(11) Anaanza kumuogopa mtu flani,a nakua hapendi kwenda sehemu flani, akimsikia mtu flani analia mpaka basi au akiambiwa kwenda sehemu labda shule anakua hataki wakati mwanzoni alikua anapenda shule.
Ukiona dalili hizi, shtuka kidogo, si kawaida, anza kumkagua mtoto wako kujua nini kinaendelea kwenye mwili wake. Kama umejifunza #SHARE na #MTAG rafiki unaweza kumuamsha mtu.