KABLA YA KUOA AU KUOLEWA USIMCHUNGUZE YEYE TU,CHUNGUZA HADI KWAO KAMA WAKO SAFI USIJEINGIA JEHANAMU NDOGO.
Usiombe tu kuoa mke mwema au kuolewa na mume mwema......lakini omba pia uoe au kuolewa katika family nzuri (njema)
Mume au mke anaweza kuwa mwema lakini family yake ikafanya hata wema wake usiuone tena.
Fikiria umeoa au kuolewa na mtu ambaye family yake ni wachawi hadi shetani anawaogopa yaani anga kwao ni kama uwanja wa mazoezi....mnaishia kuzaa watoto wenzako wanawageuza misukule tu
Unaoana na mtu kwao ubakaji ni kitu cha kawaida! Historia inaonesha babu aliwah baka, baba alibaka, wajomba wabakaji mpaka wadogo zake!!! mnazaa watoto mnaogopa hata kuwapeleka kwa kina bibi wakasalimie
Unaoana na mtu kuanzia babu zao mpaka yeye ni walevi walokubuhu! Yaani huyo mumeo au mkeo wakikaa bar na wazazi wake wanashindana kunywa bia halafu mwenzako anashinda bar mpaka asubuhi.....hiyo kesi utampelekea nani? Kama si kuambiwa "shukuru Mungu hapo kapunguza"
Unaoana na mtu baba yake ana kesi za kufumaniwa kila kunapoitwa leo na watoto kila kona ya dunia, mama mtu ndo usiseme maana ni malkia wa zinaa kitaifa.....halafu utegemee toto lao likianza michepuko na umalaya utaenda kuomba suluhu kwao???
Mnapooa na kuolewa angalieni wenza wenu na family zao pia ili mnapoanza safari muwe mnajua na balaa linalowasubir mbele. Nenda katika family ambayo unajua watakuwa msaada katika ndoa yako hata mwenzako atapokengeuka.
Siku zote kuna tabia ambazo huwa zinatembea yaani roho kamili!! Inahama kizazi hadi kizazi!! Oa au olewa katika family ambayo hata ukifa leo au kesho wanao watakuwa salama.
Usiingie kwenye ndoa kukidhi haja ya mwili,kufurahisha jamii au kutimiza wajibu,oa mwenza anayechukua nafasi yako yako kuanzia moyoni,akilini na kimajumumu.