Kosa kubwa wanalolifanya wanawake wengi wanapoingia kwenye ndoa ni kudhani kuwa ....
Kosa kubwa wanalolifanya wanawake wengi wanapoingia kwenye ndoa ni kudhani kuwa wanaweza kuwacontrol wanaume kwa kuwawekea mashariti mengi na kulazimishia mambo. Wanawake wengi wanapokua wanaingia kwenye ndoa wanakua na akili za maana, wanakua na mawazo ya kikubwa na wanawaza familia sana, wengi wako hivyo, mimi naziita akili za “Mama”.
Wanataka tuwe na kanyumba, tununue kakiwanja, tuwe na kagari, tuwe na kabisshara, mwanaume aache pombe, aache kutoa pesa kwa marafiki zake, mwanaume aache kushinda vijiweni na vitu vingine vingi. Hizi ni akili za “Mama”. Mwanaume yeye anakuwa na akili zake tu za mwanaume ambazo zote zinamuambia kitu kimoha “Mimi ndiyo mwanaume siwezi kupangiwa kitu na Mwanamke!”
Kwa maana hiyo hata kama mwanamke akimshauri kitu cha maana, kuna wanaume wanasikiliza lakini wengi wao kuna kamwanaume flani huko kichwani kake kanamuambia “Utapangiwaje maisha na Mwanamke!” unakuta mwanaume anaacha kufanya hicho kitu na mwanamke anakasirika kwakua kitu alichokua ameshauri ni cha maana. Mwanamke kama unakumbuka kuna siku uliongea na mume wako, kitu cha maana kabisa.
Mkaelewana, lakini aliporudi kabadilisha kabisa na kafanya kitu kingine! Labda mlipanga mnunue kiwanja mpandishe ukuta, lakini anarudi unasikia kanunua gari ukimuuliza hana jibu la maana. Basi si yeye ni hako ‘ka mwanaume’ kichwani kwake kanamuambia “Utapangiwaje kitu na mwanamke!” Mwanhamke hata uongee, utishie kuondoka, uweke mikwala na vingine vingi kama hako ka mwanaume kapo katakushinda.
Ubaya nikuwa wanaume hawaoni shida kuvunja ndoa zao kwa kukasikiliza tu hako ka mwanaume kalikopo kichwani kwao. Kwa mwanamke ni lazima ujue namna ya kudili nako, si kulalamika, si kununa, si kuongea sana tena hivyo ndiyo unakakasirisha hako ka mwanaume mpaka kanavimba kabisa. Kwa wenye kitabu changu sasa someni sehemu ya Tatu. Ukiisoma vizuri na ukaifanyia kazi basi mwanaume wako hatakua na shida utaweza kukaridhisha hako ka mwanaume.
Kaache kaone kana nguvu, kaache kajihisi kuwa kameshinda, kaache kashangilie, kaache kaone kuwa kamefanya maamuzi kenyewe lakini kumbe sio. Kwa mfano, kuna yule rafiki yake au mfanyakazi mwenzake ambaye unamuambia kila siku hutaki aongee naye, hutaki kumuona, hutaki ampe lift, ndugu yangu hataacha. Hako ka mwanaume hakatamruhusu, ila jifanye mjinga ataacha tu!
Nishamaliza, ni sehemu ya Tatu tu, ukiingia kwenye ndoa kabla ya kuweka mashariti basi isome kwanza ujue namna ya kudili na hako ka mwanaume.