HAJAKUACHA BADO LAKINI UKIENDELEA KULAZIMISHIA NDOA ATAKUACHA MUDA WAKE WA KUOA BADO!


Ndiyo kwanza wewe na mpenzi wako mmemaliza chuo, kuna mambo mengi ambayo mlipanga na moja wapo nikua mkimaliza chuo basi mtaoana, mnapendana sana na inawezekana hata ahsajitambulisha kwenu wazazi wanawajua. Lakini ni mmemaliza chuo, ni mwaka sasa huoni hata dalili za kukuoa, kila ukimuambia kua aje kwenu anatafuta sababu za kukwepa na kubwa kua hajajipanga.
Labda hajapata kazi bado au kuna kakazi anakafanya lakini hakana kipato kikubwa, kwakua anaweza kujihudumia na anakupa vihela vidogo vidogo unaseama nioe tu mimi nipo tayari kuvumilia chochote mpaka upate kazi! Lakini wewe labda umepata kazi na unaona mbona unaweza kujihudumia na hata kumhudumia yeye, uko tayari kujitoa na unachotaka ni ndoa lakini mwenzako hakuelewi.
Anakuambia mambo bado anataka ajipange kila siku, umepiga kelele mpaka umechoka na ushaanza kuhisi hakupendi, ushahisi labda ana mtu mwingine. Naomba nikupe habari nzuri na mbaya. Habari nzuri ni kwamba bado hajakuacha, hata kama imepita miaka miwili unatakiwa kujua mwanaume anapomaliza masomo, akili yake haipo katika kuoa bali kutafuta pesa ili aoe, yeye ili aitwe mwanaume anawaza kuhudumia familia.
Sisi ni tofauti na nyie ambao mnawaza kuolewa, unatoka kwenu unaenda kwa mtu mwingine wakati sisi tunachukua mtu tunamleta kwetu. Sijui mmenipata kua mwanaume akishamaliza masomo, kwanza atatafuta kazi, pili ataanza kujiweka imara kwamba awe na kaakiba kua hata akioa basi aweze kuhudumia mke. Mwanaume anayejielewa haoi tu wakati hana kazi ya uhakika wa kuhudumia familia au aoe tu kwakua mke ana kazi.
Hapana mwanaume anayejielewa anajua jukumu la kuhudumia familia ni lake hivyo hata kama mwanamke ana kazi hawezi kumuoa mpaka yeye awe na kazi na uhakika wa kumhudumia hivyo inaweza kuchukua mwaka, miaka miwili hata mitatu. Sasa kama uko kwenye mahusiano na mwanaume wa namna hii vuta subira mpaka aweze kujitegemea, akipata kazi inamtosha kula na kulisha familia asipokuoa hapo ndiyo kua na shaka.
Akisema mpaka ni jenge au mpaka ninunue Gari hapo ndiyo kua na mashaka anaweza kua anakupotezea muda. Lakini nikupe habari mbaya pia kama bado hajapata kazi au amepata lakini haijaanza kumfanya kujitegemea, kelele zako za kila siku za nioe, lini unakuja kwetu zitamkimbiza. Kwanza ni kwakua utakua unamsumbua, unamnyima amani ya kufanya mambo yake, lakini pili nikwakua ataona kama umepagawa juu yake.
Unamtaka sana na huna maisha bila yeye hivyo atakukinahi mapema. Kama bado hajajua kukuoa badala ya kila siku kuimba njoo kwetu hembu kua bize na maisha kua bize kutengeneza kwako, uwe na kitu chako ili hata asipokuoa na wewe usipate hasara ya kusubiri. Mwanaume akiona unajielewa nirahisi kukuoa kama anakupenda kwani anajua mtasaidiana lakini kama kila siku ni kelele za njoo kwetu atajua ni kimeo utamsumbua ndani ya ndoa.
Hembu kua na mipango yako ya maisha zaidi ya ndoa, kwamba kama umemaliza chuo umepata kazi hujafika mwisho bado, unatakiwa kujenga, kufungua biashara na kutengeneza maisha yako. Wakati unamsubiri yeye ajipange, jipange na wewe kwani hata si lazima akuoe yeye. Ukiona kama haelekei, yuko vizuri lakini analeta sababu ambazo si za msingi ndiyo unaweza kumuambia kwa heri, umepoteza muda lakini si fursa za kimaendeleo.
May be an image of 6 people, people standing, flower and outdoors


DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA