KWANINI KADIRI MIAKA INAVYOZIDI KWENDA NDOA ZINAPUNGUA...WAOAJI WANAKUWA WACHACHE..
Zipo sababu nyingi sana kadiri tutakavyokuwa tunapata muda tutajifunza.. Leo tutajifunza moja..
1: Hii ni kwa sababu vijana wengi wa kike wamekubali kuchukua majukumu ya kindoa kwa mtu ambae ni boyfriend tu na sio mume... Unapochukua majukumu ya kuwa mke kwa boyfriend unamfanya mwanaume yule kujisahau...
Ebu jaribu kutazama mwenyewe..
Boyfriend wako akitaka kufuliwa upo unafua.. akitaka sex upo unampa tena wakati wowote.. akitaka kupikiwa upo unampikia.. chochote anachotaka kutoka kwako anapata...
Je niambie mtu huyu atakuwa na haraka ya kukufanya rasmi kuwa mke?
Ukweli ni kuwa hapana hawezi kuwa na haraka hiyo ..hii ni kwa sababu anapata kile ambacho wanandoa ambao wameshaoana rasmi wanapata.
Nakukumbusha in case ulikuwa umesahau kuna boyfriend na girlfriend, kuna wachumba, mwisho kabisa kuna mke na mume.
Na kama ulikuwa haujui wengi waliochukua majukumu ya kuwa mke kwa boyfriend wake hawakuolewa ni wachache sana kati ya 100 watano tu waliolewa .. 95 waliobaki waliachana mwanaume akaenda akaoa yule mwanamke ambae alimwambia ukiniitaji kuwa mkeo nioe kwanza then nitafanya kila kitu ambacho mke anastahili kumfanyia mume wake... Kwa maana nyingine mwanaume anapenda mwanamke mwenye misimamo yake.
Nakukumbusha tena..
Don't be a wife to your boyfriend, but what you need is to be a good girlfriend to your boyfriend... Hii inatosha kabisa.