Mambo 9 Muhimu Kuhusu Kulea Mimba ya Watoto Mapacha

 Image result for dalili za mimba ya watoto mapacha


Kama  kuwa unategemea kujifungua watoto mapacha na hujui nini kinachokuja mbeleni basi hauko peke yako. Wanawake wengi ambao wanategemea kujifungua mapacha huwa hawajui nini kinacho kuja mbele yao ila haimaanishi hawawezi kujifunza.
Mama anaweza svika mamba ya mapacha wwili,watatu,wanne na kuendelea.,Ila mapacha wawili huwa ndio haswa wamama wengi hujifungua kwa wingi.Hapa nina taarifa mbali mbali ambazo zinaweza kukupa mwanga tu kidogo juu ya mambo ambayo unaweza kukutana nayo wakati unalea mimba yako ya mapacha.
Utakua Unatakiwa Kwenda Hospitali kwa Ajili ya Uchunguzi Kila Mara.
Mimba ya mapacha inahitaji uangalizi wa hali ya juu kuliko mimba ya mtoto mmoja. Kufanya uchunguzi wa ultrasound unaweza ukafanywa kila mara kwa ajili ya kuangalia jinsi watoto wanavyokua .
Kujisikia Kuumwa Mida ya Asubuhi. Morning Sickness.
Ukiwa na mimba ya mapacha una hati hati ya kujisikia kuumwa mida ya usubuhi. Kuumwa huku huwa kuna ambatana na kutapika mara kwa mara kwa sababu umebeba watoto wawili tumboni kwa hiyo kuna homoni ambazo zitapelekea wewe kujisikia kutapika.
Good news ni kwamba hii hali huwa sio ya mda mrefu, inakuwepo kwa mda wa week 12 mpaka 14 baada ya mimba kujulikana.
Kitu kingine ni kwamba mama ambaye amebeba mimba ya mapacha huwa wanapata maumivu ya mgongo na hupata shida  kupata usingizi kwa hiyo wanashauriwa kupumzika kwa sana na kuacha kufanya kazi ngumu ngumu ambazo zinawaumiza mgongo. Vile vile baada ya kujifungua huwa kuna hati hati ya kutokwa na damu nyingi ambayo huwa inapelekea kupungiwa na damu mwilini kwa hiyo ni vema ukajua hilo.

Unatakiwa Utumie Kiwango Cha kutosha Cha Folic Acid

Pale mama anapojua sasa unamimba ya mapacha ni vizuri ukatumia Folic Acid ya kutosha isiwe pungufu ya 1miligram kwa siku.Bila kusahau kula mboga mboga na matunda kwa wingi hii itakusaidia kutengeneza damu ya kutosha inayohitajika kwako na watoto wako ,ili kutimiza safari yenu salama.

Utawasikia Watoto Wakipiga Piga Tumbo Mapema.
Si unajua ukiwa umebeba mimba ya mtoto mmoja huwa kuna wakati unamsikia kabisa akipiga piga tumbo na miguu yake, basi ukiwa na mimba ya mapacha hawa utaanza kuwasikia mapem zaidi baada ya week 18 mpaka 20 za ujauzito. Kama ni ujauzito wako wa kwanza basi wala usishituke ila kama ni mara yako ya pili basi hii mitikisiko ya tumboni utakua unaijua. Watoto wanatingishika ndani mpaka unajiuliza wanapigana nini!
Ukiwa na Ujauzito wa Mapacha Unaweza Kuongezeka Uzito.
Ukiwa na watoto wawili tumboni uzito lazima uongezeke. Yaani utaongezeka uzito kwa sababu kuna watoto wawili umewabeba tumboni, na bado haijajulikana kisayansi kwa nini uzito huwa unaongezeka kwenye mimba za mapacha.Ila kwenye mwili wa mama mahitaji ya motto yanakuwa ni double mfano mlo wa mama mjamzito wa kawaida anaweza akala kawaida ila mama mapacha akala zaidi sababu ya ni wawili.
Kwa ujauzito wa kawaida mama anaweza kuongezeka kilo 11 na kwa mama mwenye ujauzito wa mapacha anaweza kuongezeka kilo 13 hadi 15 ila isizidi kilo 20 maana hiyo ikifika basi inakua ni hatari kabisa. Watoto mapacha mahitaji yao yanaongezeka na ndio kumfanya mama kutanuka hata mwili mfano placenta zinahitajika 2,kiwango cha amniotic fluid kinahitajika mara 2 n.k
Mama mwenye mapacha anakiwa kujitahidi asiwe na uzito mkubwa,jaribu kufanya mazoezi mara kwa mara kama ya kutembea,kuogelea n.k

Hujifungua Mapema
Ujauzito wa mapacha  huwa wanaweza kujifungua mapema kuliko ilivyokawaida. Kwa kawaida mama anajifungua akiwa  amebeba mimba kwa week 40 huku mama mwenye ujauzito wa mapacha anaweza kujifungua na weeks 36 au 37 za kubeba ujauzito.
Kama mtoto amezaliwa baada ya week 34 basi hapo hamna shida sana kuliko aliyezaliwa kabla ya week 34

Kisukari Cha Mimba

Mimba ya mapacha inauwezo mkubwa wa kumfanya mama kupanda kwa level ya sukari.Hii inatokea tu kipindi cha ujauzito kutokana na mabadiliko ya mwili na homuni kujibadilisha.Ila kisukari cha mimda kinatibika mapema iwapo mama atakuwa anahudhuria clinic kwa wakati muafaka na wakagundua tatizo.

Kifafa Cha Uzazi

Kifafa cha uzazi ni kawaida haswa kwa mama wajawazito hii inatokana na mama anapokuwa na kiwango kikubwa cha protein kwenye mkojo,kuwa high blood pressure hive vote zinapelekea mama kupata kifafa cha uzazi.Kuna dalili za awali mama atazipata kwenye mwili wake kama kuvimba miguu na mikono.Unapoona dalili yoyote ile usio ielewa wahi hospital.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA