Umezaliwa na uwezo mkubwa sana kuliko unavyojifikiria lakini kwa bahati mbaya unatumia sehemu ndogo sana ya uwezo wako ambao umezaliwa nao
Hakuna mtu ambaye amezaliwa asifanikiwe maishani lakini tofauti ya watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa ni namna wanavyotumia akili zao
Je unajua akili yako ndio injini ya mafanikio yako?
Ndio akili ni injini ya mafanikio yako kwa sababu ndani ya akili yako ndio msingi wa mawazo kuzaliwa, ndoto kuzaliwa na maono kujengwa
Mafanikio yako yamebebewa sana na namna unavyotumia akili yako kwa maana akili ndio inakupa mamlaka ya kufanya jambo au kitu fulani kwa muda gani na mahali gani (Kusudi la kuzaliwa kwako)
..... Je unajua watu wote waliofanikiwa wanatumia akili kwa maana kuongeza ubunifu na kujitofautisha na watu wengine pamoja na nguvu
Tazama Kanuni hii
Work Hard + Work Smart= Success (Kufanya kazi kwa kutumia Nguvu + kufanya kazi kwa kutumia akili = Mafanikio)
Unajiuliza nifanye nini ili uitumie akili yako kukupa mfanikio...
Kuitumia akili yako ipasavyo ili ufanikiwe kwenye kitu unachofanya, Anza kufanya mambo yafuatayo;
1. Ongeza kiwango cha kujitambua wewe ni nani (Tazama ukurasa wa LEMBRIC SWAHILI QUOTES utakusaidia kujitambua kwa kiwango cha juu)
2. Jenga tabia ya kujifunza kila siku kwa kuongeza maarifa (Tafuta Kitabu Cha Power of the subconscious mind kitakusidia kujua akili yako inafanyaje kazi)
3. Ongeza kiwango cha kujifanyia tathimini binafsi (Self evaluation)
4. Ongea na akili yako (Meditation)
Tumia akili yako kujenga maisha yako kwa kuongeza maarifa kila siku ili ujue namna ya kufikiri fikra chanya na kuwa na taswira chanya ya maisha yako na mafanikio ambayo unataka kwenye maisha yako
Tumia akili yako kuboresha maisha yako, akili ndio mtaji mkubwa wa kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa kwenye kitu unachofanya inawezekana sana
Injini ya mafanikio yako ni akili yako
Kauli Mbiu: “MAISHA NI KUTHUBUTU”
_____
ZINGATIA: “Unahitaji sana kujenga sifa ambazo mtu anayetaka mafanikio anapaswa kuwa nazo ili ufanikiwe kwenye kitu unachofanya”
___________