KWENYE MAHUSIANO KUNA VITUKO
Mnaweza kuwa ma-girlfrends watatu kwa mkaka mmoja, msichana wa-kwanza nd'o anapiga pini balaa akijua anaolewa yeye halafu anakuja kuolewa yule wa tatu, au mnakuwa wakaka watatu kwa mdada mmoja na hamjijui, huyu wa-kwanza hadi ndoto za harusi anaota halafu ndoa anakuja kufunga mkaka wa tatu ambaye hata alikuwa hajiamini kama mzigo ni wakwake.
Kwingine mnakuwa wanawake wanne kwa mkaka mmoja na hamjuani, kila mmoja anajua ni mgombea wa jimbo, ghafla mnasikia kaka anaoa halafu anaoa ambaye hata kwenye listi ya wanne hakuwepo.
Yani staili zakuingia kwenye ndoa ni vululuvululu, kila mtu ananjia yake, sasa ishu iko kwenye jinsi gani mtaishi pamoja kwenye hiyo ndoa, hapo ndipo dagaa hujua kwamba sato nae ni samaki kama yeye ila wana-tofauti kwenye umbo tu na hapo ndipo wanasheria wanapata wateja wao wa talaka na sisi washauri tunapata wakwetu.