ZINGATIA YA FUATAYO ILI KUEPUKA MAUMIVU WAKATI WA KUACHANA.
1. Mwamini Mungu maana ni yeye tu asiyebadilika ila Mwanadamu anabadilika.
2. Fahamu kuwa una-date Mtu na sio malaika, anamapungufu na anauhuru wa maamuzi.
3. Kutofaa kwa huyo mpenzi wako haikufanyi kutofaa kwa ulimwengu mzima. Dunia inawatu zaidi ya Billion 7, hivyo akiondoka yeye kuna wenzake Billion 6+ wanakusubiri.
4. Mahusiano sio Ndoa na yameruhusiwa kuvunjika. Hivyo kuachana sio jambo la ajabu wala la aibu.
5. Inawezekana kuvunjika kwa hayo mahusiano ni ishara kuwa Mungu anakuepusha na janga kubwa zaidi huko mbele. Mshukuru Mungu na umwamimi.
6. Samehe, achilia, linda amani ya moyo wako kwani maisha bado yanaendelea.
7. Jipambe, vaa, pendeza, kula vizuri na upate muda wa kupumzika kwani hujafiwa ni kama tu umeacha kazi Kampuni moja kwenda nyingine.
8. Acha kujilaumu kwa yote uliyomfanyia kwani ilikuwa sehemu ya Mchakato wa mahusiano, hata asingekuwa yeye bado ungefanya kwa mwingine. Hakuna sababu ya kuchanganyikiwa.
9. Hatma yako iko mikononi mwa Mungu na ndiye anayeamua kesho yako. Usiruhusu mwanadamu akashikilia amani yako. (Yeremia 1:5, Isaya 46:10, Yohana 14:27)
10. Ni mtu aliyeondoka, bado alichokukuta nacho amekuacha nacho. Kilichomvutia bado unacho atakuja mwingine so acha aende kwa amani.
Chukua muda wa kupona nafsi yako, usiingie kwenye mahusiano mapya ukiwa bado unamaumivu ya uhusiano uliovunjika, hakikisha umepona kiasi hata ukimuongelea hausikii uchungu ndani yako. Hapo uko huru kuanza mahusiano mengine.
NB: Mkaka kama wakati unamtongoza huyu Dada ulienda naye hotel ya kimataifa akala ndio ukatema sera zako. Kwenye kumuacha pia ni vizuri ukamrudisha kule kule na ukamuacha kwa amani. Sio kwa meseji kwenye simu "IT IS OFFICIALLY OVER" bila maelezo ya msingi. Utaua Mtoto wa watu. Man up and be a gentleman.
*Kwa wanawake usiende kuachana na mwanaume chumbani kwake. Ni hatari kwa Afya yako.
Pia epukeni kupeana zawadi kubwa kubwa kama Nyumba na magari kabla hamjaingia kwenye Ndoa, huwa yanazidisha maumivu hasa ukimuona Ex wako na mtu mwingine wanapita wakiendesha jasho lako na wewe uliyenunua umeachwa. Loh!!!!!!!!!!!
ALIYE NA SIKIO NA ASIKIE.
ZINGATIA HILI!!!
Unaweza kumpoteza Mwanamke bora, mwenye baraka kwa sababu tu ya Mwanamke mzuri mwenye mikosi kibao aliyewashinda wanaume wenzako tabia.
Kama uko hivyo basi utakuwa na haiba ya fisi kula mizoga na kutafuna mifupa iliyowashinda mbweha ni sawa lakini angalia usipate laana ya mwanamke wako aliyekuheshimu,kukuvumilia na kukuthamini wakati wote wa maisha yenu,chozi la mwanamke lililo haki halimuachi mwanaume salama.
Chozi la mwanamke Asie na Hatia Ni Laana kuliko Unavyofikiria
Usimpe Nafasi Mwanamke akamwaga Chozi Lake Akimlilia Mungu Juu ya Mateso na Manyanyaso Unayomfanyia
Kama Humpendi Mwache kwa Wema, Usimtumie kwa Maslai yako Binafsi
Mapenzi Ni Zawadi kutoka kwa Mungu, Usiyatumie kumuumiza Mwenzio
Achana nae ..
Unalala, haupati usingizi juu ya mtu ambae huenda amelala na mtu mwingine muda huu kwa amani tele.
Achana nae!
Unaangalia simu yako sasa hivi ukisubiri text ya mtu ambae unamuona yuko online anachati na mtu mwingine kwa furaha zote..
Achana nae!
Unaweka status za huzuni WatsApp kuonesha namna gani unavyoumizwa, wakati yeye yuko busy anamfikiria mtu mwingine, anampa furaha mtu mwingine, anamuweka status kuwa anampenda sana na wewe amekuficha usiweze kuiona status.
Achana nae..!
Kweli unalia juu ya mtu ambae anamfurahisha mwingine?? Sio sawa bhana, hebu sikiliza, kama wewe sie ambae anakujali, basi hutakiwi kuwa na wasiwasi tena, wewe sie wake. Yuko mtu mwingine badala yako.
Ni ngumu, inauma sana na sio rahisi lakini kaza moyo, vaa moyo wa ujasiri, na hebu achana nae!!
Ipo siku, utakuja kuwa na mtu atakaekusahaulisha magumu yote uliyopitia!!
MEET ME AT THE TOP
*TABIA 12 ZITAKAZOKUFANYA UWE MWENYE FURAHA MAISHANI*
*1. Samehe*
Samehee hata wasiostahili kusamehewa.
Usikubali kuwa na kinyongo au ugomvi na mtu yeyeto.
Jifunze kupotezea.
Usimjibu kila mtu kila kitu.
Hata ukimya ni majibu.
*2. Jiamini*
Hakuna lisilowezekana chini ya jua. Anza sasa.
Wenye imani wana amani kila wakati.
Wenye imani wanakuwa na uhakika wa kile wanachokitarajia.
*3. Jifunze*
Mungu hakumuumba mtu kuweza kila kitu wakati wowote.
*4. Jipende*
Umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Usijidharau wala kujishusha kiwango. Jitamkia mambo mazuri kila wakati.
*5. Tabasamu*
Furaha ni tiba ya moyo
Jifunze kuhesabu baraka ambazo Mungu amekupatia itakisaidia kutabasamu kila wakati.
*6. Usihukumu*
Hakuna mwaminifu chini ya jua. Kila mmoja anakosea hata wewe huwa unakosea na kuwakosea wengine.
*7. Jiheshimu*
Mfumo wa maisha yako ndio utakuwa msaada kwa wengine. Wewe ndiye utakayewafanya wengine kukutafasiri.
*8. Panga malengo*
Malengo ni taa, dira, ramani,kesho, mwelekeo, matumaini. Usiishi pasipo kujua kesho yako au pasipo kujua unapoelekea.
*9. Fanya Ibada*
Mahusiano yako pamoja na Mungu ndio chanzo cha kubarikiwa kwako.
*10. Kula vizuri*
Mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu kuwa makini sana kwenye ulaji wako. Usile chochote unachotaka Bali kula chochote kinachohitajika mwilini mwako.
*11. Kuwa mkarimu*
Hukuja duniani na kitu Bali vyote ulivyonavyo chanzo chake ni Mungu. Lakini pia vyote utaviacha duniani siku yako ya kufa itakapofika. Ukarimu ni akiba ya baadae kwa ajili yako na kizazi chako.
*12. Kuwa mwenye shukrani*
Ukitambua na kutafakari ulipotolewa na huyu Mungu hakika hautashindwa kusema asante kwake.
Mshukuru Mungu kwa kila jambo hata kama mengine yanaenda vibaya endelea kumwambia Mungu asante...........
Samehe ili na Baba yako aliye mbinguni akusamehe.
Samehe ili hayo majeraha na Maumivu yatoke moyoni
Samehe ili upone , Samehe ili usifunge milango ya Mungu kusema nawe
Samehe ili Roho mtakatifu aweze kufanya kazi yake ndani yako
Samehe ili ujiepushe na magonjwa yasababishwayo na kurundika vitu ndani ya Moyo
Samahe ili Uishi miaka isiyo ya magonjwa ya moyo,presha ,msonho
Wa mawazo
Samehe ili Uwe na Nuru mpya
Samehe tu maana ata wewe ni mwanadamu ulishakosea na utakosea tu
Samehe maana amesema yeye kuja kwake atujui anakuja kama mwivi je? Akikukuta umebeba hayo umeshindwa kusamehe utaenda kweli
Usiangalie ni nani wewe samehe atakama ni yule ulimwamini kuliko naye pia ni mwadamu we msamehe tu
Kuna mtu naongea naye ,Nakuombe Mungu akuponye
Mwalimu Bemasha
MTUMIE MWENZAKO PIA AWEZE INGIA KWENYE GROUP AMBALO NI MSAADA SANA KWAKE NA MAISHA YAKE WEWE MWENYEWE SHAHIDI LIMEKUSAIDIA KWA KIASI GANI ILI GROUP