ULIPATEJE MKOSI LAANA YA KUTOKUOLEWA HADI LEO SOMA

Mbona mama zetu waliwavumilia baba zetu ako kapepo umekatoa wapi😆😆😆
wewe endelea msumbili mwenye mahela.....kwa mwaka mdada anatongozwa na watu zaidi ya 50 kwa mwezi sio chini ya wanaume 10 ....amekuwa mkubwa tuanze anamiaka 18 saizi anamiaka 28 .... ndani ya miaka 10 kila mwaka anatongozwa na wanaume 50 tangu anakuwa hadi leo katongozwa na wanaume zaidi ya 500 na anasema sijaona mwanaume mkweli...kweli katika 500 ajawai tokea mkweli Mungu anakuletea mapepo hapana Mungu hana tabia iyo yawezekana alikuja kijana wa kawaida sana ambaye Mungu alisema huyu ndio mumeo ukamzalau ukataka wenye sixpack ....
ingia katika toba aise usizalau watu ukute alikuja aliyetakiwa kukuoa ukamzalau......ukawe karibu sana na Mungu
Unaweza kuolewa na mtu ana Range Rover na bado ukapanda Daladala/Matatu/Tax (public transportation) au Uber, Lyft, Taxify kwenda kwenye shughuli zako. Unaweza kuta ana nyumba kubwa na magari uwani ila yakawa yake na sio yenu. Usikimbilie vitu angalia sana utu.
Unaweza kupata Lawyer, Daktari, Banker, au Mfanyabiashara ambaye hela ni zake na sio zenu, na ukakutana na Mishentown hana dili ya kueleweka ila kila anachopata analeta nyumbani. Usikimbilie vitu angalia sana utu.
Wako watu kwenye Ndoa za Kifahari na maisha ya maigizo, hawana amani, hawana furaha. Wapo wanawake wanapigwa na kufanyiwa ukatili na unyanyasi Mkubwa sana ila wanashindwa kushtaki kwa kulinda status za wanaume zao. Usitishwe na Majumba makubwa na magari ya kifahari, tafuta mahali utapendwa kweli na kupata amani ya moyo. Kuna watu hawalali usiku kwa sababu ya majeraha ya moyo. Na kuna wengine wana maisha ya kawaida sana ila wanaishi mbinguni duniani.
Ni kweli mnaslogan mpya kuwa “hapa hapendwi mtu inapendwa pesa tu”, ila kuna watu wamezikimbia hizo pesa na wamerudi kupanga uswahilini.
Ni afadhali asiye na kitu ila anakupenda na anapambana na akipata mnashea kuliko mwenye kitu asiyekuthamini, anakunyanyasa. Unafanyishwa ngono kinyume na maumbile, unadhalilishwa na kuteswa. USIKUMBILIE VITU ANGALIA SANA UTU. USIPOKUWA MAKINI NDOA INAWEZA KUKUKOSESHA MBINGU.
(a) Jijue Wewe, Mjue Mchumba Wako na Mizimu au Walozi Katika Familia Yake Kabla ya Kuingia Kwenye Ndoa.
(b) Jijue na Mjue Sana Mume/Mke Wako na Mizimu au Walozi Katika Familia Yake ili Ujue Namna Ya Kuishi Naye Kwa Amani.
(c) Ishi na Mume/Mke Wako Kwa Akili 4
(d) Ishi na Ndugu Za Mume/Mke Kwa akili
Bila msaada wa Mungu ndoa yako ni bure tu maana unaolewa na mtu usie mjua naujui jinsi ya kushughulikia ulimwengu wa roho wa upande wako na wake
May be an image of 2 people and people standing

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA