ACHA KULIPIZA KISASI
ili kuww na mabishano lazima kuwe na watu Wawili wanozungumza lakini mmoja anaponyamaza na kusikiliza badala ya kuzungumza ,mabishano huisha.kwahiyo ,epuka kumjibu mwenzako unapo kasirishwa.Dumisha heshima yako kwa kujizuia .kumbuka ,kuwa na amani katika familia Ni muhimu zaidi kuliko kushinda mabishano.
ELEWA HISIA ZA WENGINE KATIKA FAMILIA
kumsikiliza mwenzio kwanza kwa lakini ukiwa na hisia -mwenzio bila kumkatiza au kumhukumu kunaweza kutuliza hasira na kudumisha amani .Badala ya kumshuku mwenzako ,tambua hisia zake usifikiri ana nia mbaya wakati amekosea tu kwa sababu ya kuto kamilika.Huenda akasema maneno yenye kuudhi bila kufikiri au kwa sababu ameumizwa hisia na si kwa sababu ana kinyongo au analipiza kisasi.
JIPATIE NAFASI YA KUTULIA
ukikasirika, huenda ikafaa uondoke kwa busara ili utulie kidogo unaweza kwenda kwenye chumba kingine au ukatembee had I utakapo kuwa sawa.kufanya hivyo Ni sawa na kumnyamazia mwenzako. badala take huenda Ni nafasi nzuri ya kusali ili Mungu akupe Subira ,ufahamu,na uelewaji.
FIKIRIA KWA MAKINI NI NINI KINACHOHITAJIKA KUSEMWA NA JINSI YA KUKISEMA
Hakuna faida ya kutafuta maneno ya kujibizana na mwenzako badala take ,jaribu kusema jambo litakalotuliza hisia zilizoumizwa za mpendwa wako.N badala ya kumwamulia mwenzako hisia zake.mwombe ajieleze na nashukuru kwa kukusaidia kuelewa hisia zake.
ZUNGUMZA KWA SAUTI YA CHINI KWA NJIA INAYO ONYESHA UNATAFUTA MAPATANO
mtu mmoja katika familia anapokosa Subira anaweza kumsha hasira ya mwenzake epuka kejeli,matusi,au kuzungumza kwa sauti ya juu,hats ikiwa umekosewa.Epuka kuwalaumu wengine kwa kusema mambo kama vile "wewe hunijali" au " wewe hunisikilizi kamwe" badala take mweleze mwenzio wako kwa utulivu jinsi ambavyo mwenenendo wake ulivyokuathiri (naumia unapo....)hupaswi kamwe kumsukuma mwenzako ,kumpiga kofi ,teke, au kumtendea jeuri ya aina nyingine.pia hupaswi kumtukana,kumdhihaki,au kumtisha mwenzi wako.
OMBA MSAMAHA UPESI NA UELEZE UTAKACHO FANYA ILI KULEKEBISHA HALI
usiache hisia zisizofaa zikufanye usahau kwamba lengo lako kuu Ni kufanya amani.kumbuka kwamba hamfaidiki mkilumbana lakini mkifanya amani wrote mnafaidika kwahiyo kubali kosa lako hata ikiwa unasadiki kwamba haujakosea .unaweza kuomba msamaha kwa sababu ya kukasirika ,kwa kutenda ya siyo faa au kwa kumkasirisha mwenzako bila makusudi .kudumisha amani kati yenu Ni muhimu kuliko bishano na ukiombwa msamaha use Tayari kusamehe.