DALILI NA ALAMA 5 ZITAKAZO KUONYESHA KUWA MUMEO ANATOKA KIMAPENZI NA Mwanamke MWINGINE
01 ANACHELEWA KUTOKA KAZINI:
Mumeo kila siku anarudi kutoka kazini katika muda sahihi, na ghafla utaratibu huo ukaanza kubadilika akawa anachelewa bila sababu wala udhuru wa kueleweka.
02 ANACHUKUA MUDA MREFU KUJIBU UJUMBE WAKO:
Ikiwa umezoea kwamba anajibu sms zako haraka hata akiwa busy sana na ghafla akaanza kuchelewa kukujibu, hiyo inaweza kuwa ni dalili ya kutumia muda wake kusuhubiana na mtu mwingine.
03"ANAACHA KUFANYA TENDO NA WEWE:
Mwanaume aliyeshiba mapenzi hatotaka kukidhi mahitaji yake ya kimwili hata na mkewe. Hivyo, tazama mwenendo huo vizuri.
04"MWENENDO WAKE WA KITANDANI UNABADILIKA:
Ikiwa ghafla kuna mwenendo mpya kitandani hilo linaweza kusababisha shaka. Hapo unatakiwa kujiuliza ameyatoa mambo hayo mapya? Je, anayafanya pamoja na mwanamke mwingine?
05' ANAPORUDI NYUMBANI AKAENDA MOJA KWA MOJA BAFUNI:
Ikiwa ana mazoea endelevu ya kuingia bafuni mara tu anaporejea nyumbani, hiyo inaweza kuwa ishara ya kuficha ushahidi wa usaliti wake kutoka kwa mwanamke mwingine. Lakini hiyo haina maana kwamba lazima atakuwa ametoka kufanya mapenzi na mwanamke mwingine, isipokuwa iwapo ishara nilizozitaja mwanzo zitakuwepo ndizo zitakazokupa uhakika wa shaka yako