Kuna wakati huwa najiuliza sisi wanaume au vijana akili zetu zinafanya kazi kweli au hapana
Kuna watu humu watu wa ajabu Sana unasikia Mimi siwez kuoa mwanamke mwenye mtoto Kwan Kuna mtu kakulazimisha kuoa mwanamke mwenye mtoto
Unaona mwanamke hana mtoto mnagombana kila wakati kisa Ana michepuko kibao
Naomba kusema Jambo moja wengine humu pamoja na kuwakejeli wanawake wenye watoto lakin ndio vinala wa kuwatundika mimba watoto wa watu na kuwakimbia kazi yao kutembeza mkia wao wa mbele kwa wanawake acheni upumbavu kuwatukana wanawake
Mbona wewe umelelewa na baba mlez Kwan hukusema ukiwa huko Kama huwez kuoa mwanamke mwenye mtoto acha kuwachezea watoto wa watu acha kuwapanua mapaja yao
Naomba kuelewa kuwa hakuna mwanamke anapenda kulea watoto wakiwa peke yako ila porojo za sisi wanaume ndio chanzo hakika japo wapo wanawake ambao hawana msimamo anakuwa na wanaume 3 au mmoja ila asilimia kubwa usaliti upo na sisi wanaume hatupendi wengi tumetanguliza tamaa mbele
Siku moja nitakuwa na familia nitakuwa na mke ila siwez kuwa na dharau hata siku moja ktk yote ndio maomb kwa Mungu anipe neema na hekima ya kuwa na busara
Wanaume tukumbushane kuwa maisha ni fumbo tuache Tabia ya kuwachezea watoto wa watu kumbuka ipo siku nawe utakuwa mzazi vipi wakimpa mwanao mimba na kusepa utajisikiaje maisha haya tusiumizane tusaidiane na kujaliana maisha ni safari ndefu Sana
Unamharibia mtoto wa watu maisha unakuja huku eti sitaki mwanamke mwenye mtoto uliyempa mimba unataka Nani auoe au unataka awe mwanamke wa kudanga achani kujitoa ufahamu sio kila mwanamke anapenda kuzaa akiwa kwao ila wengi wetu sisi wanaume tunaumiza watoto wa watu
Ipo siku mtakuja kunielewa namaanisha Nini