MADHARA MABAYA YA KIROHO, MAWILI UTAKAYOPA BAADA YA KUFANYA UASHERATI/UZINZI...


Kabla ya kusonga mbele hatuna budi kufahamu maana ya maneno haya UZINZI na UASHERATI.
UZINZI hichi ni kitendo kiovu ambacho kinafanywa na mwanandoa kati ya mwanamke au mwanaume,kufanya ngono tofauti na yule mke au mume wake wa ndoa...
UASHERATI ichi ni kitendo ambacho kinafanywa na mtu ambae ajaoa au kuolewa.
Mpaka hapo tumejua maana ya maneno hayo tupige hatua sasa kujua madhara haya ya kiroho ambayo mtu atapata ikiwa atafanya vitendo hivyo...
Lazima tujue Mungu wetu ni wa utaratibu na pindi unapofanya jambo lolote kinyume na utaratibu wake hilo linakuwa ni dhambi,,,,Katika swala hili MUNGU amemtaka kila mwanaume au mwanamke kuwa na mume au mke kwa sababu ya zinaa,ila wengi hawataki kufuata utaratibu huo wanatumia short kati zao na matokeo yake yanakuwa mabaya sana sio kiroho tu na kimwili pia ,ila kwa leo siko hapa kuzungumzia madhara ya kimwili bali nitazungumzia Kiroho zaidi... Kama ifuatavyo..
1 KUWA MWILI MMOJA..
Tendo la zinaa liwe la uasherati au uzinzi linawafanya kuwa mwili mmoja ,katika ulimwengu wa Roho,sasa usione umefanya tu ukondoka uwe na uhakika ww ni mwili mmoja na huyo uliyefanya nae huo uchafu wako,,,EBU TUONE HII KUWA MWILI MMOJA INA MAANA GANI,,YESU KRISTO NI KICHWA CHA KANISA,MWILI NI KANISA NA VIUNGO NI SISI,,hii ina maana sisi sisi tulio mwamini Yesu Kristo ni mwili mmoja naye..
27 Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.
1 Wakorintho 12:27
Unaona maandiko hayo 👆👆👆,,sisi tu mwili mmoja na Yesu kwa maana ya kwamba zile baraka zote za Yesu tutazirithi kutoka kwake kwa sababu tumekuwa mwili mmoja naye katika ulimwengu wa Roho ,kwa maana nyingine kama Yesu angekuwa na laana,mikosi na sisi pia tungezirithi izo kwa sababu tu mwili mmoja...
3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Waefeso 1:3
Unajua kwamba kila unapozini na mwanaume/mwanamke yyte nafsi ya huyo mtu hubaki kwako na baadhi ya mapepo huingia kwako, hii mara nyingi itakuletea tabu sana kwenye ndoa, sababu itakua mwenza wako akiwa mbali unammic lkn mkionana tu jambo dogo tu amani haipo ni ugomvi kwenda mbele , sio kwamba hakupendi ni hizo nafsi ndio zinagombana ndani yenu kila nafsi inahisi imedhurumiwa mke/mume so zitaanza kupigana, na kupigana kwa hizo nafsi ndani yenu matokeo yake ni ugomvi wenu ninyi wawili, hapo mtasuruhishwa mtaombewa ,mnatulia siku mbili tu ya3 moto uleule, labda mkutane na Nabii wa MUNGU alione hilo awaambie namna ya kujinasua hapo , Sasa jiulize we mwenyewe umezini na wangapi na mara ngapi?
Shetani uwa hapendi watu wa Mungu wajue siri zake... Maana atakosa wafuasi...... Na ukiijua kweli kweli itakuweka huru.... Maana Mungu Alisema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa kama haya ya sexual transmitted demons
Soma 2 samweli 11:4Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi
Saudi alipo lala na mke wa uria mwanamke alitakasika juwa kila unapo zini unachukuwa Roho toka upande wa 2 ndio maana uzizi kuacha sio kitu chepesi maana ni maroho umebeba toka watu tofauti
TOBA YA KWELI
Umeona maandiko hayo👆,kumbe kuwa mwili mmoja na Yesu tunarithi baraka zote kutoka kwakwe kwa sababu tumekuwa mwili mmoja naye ..
Hivyo hivyo unapofanya uasherati au uzinzi ,unakuwa mwili mmoja na huyo mwanaume au mwanamke...
Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
1 Wakorintho 6:16
Kama alikuwa na laana,mikosi,balaa zote tarajia kupata hayo na wewe maana ni mwili mmoja tayari,unakuta bint au kijana amezini na wanaume zaidi 100,unakuta unatembea na maroho mabaya,unashanga tangu umelala na binti au kijana fulani mikosi,balaa ,magonjwa hayaishi kwenye maisha yako,tangu umelala na binti au kijana fulani,umekuwa na roho ya umalaya usio kuwa wakawaida mpaka unajishangaa,dawa ni moja ni kutubu kwa maanisha na ujiungamanishe na Yesu Kristo tu...
2. ZIWA LA MOTO..
ndugu yangu hili ndo dhara baya zaidi ambalo usitamani kulifikia maana ni mateso mabaya ya milele mfano wake hakuna chini jua,usifurahie kufanya tu uovu huo bali lazima ujue kuna hukumu na hukumu iyo ni kutupwa katika lile ziwa liwakalo moto na kibereti...milele yote ..
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na WAZINZI, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Ufunuo wa Yohana 21:8
Mshahara wa dhambi sehemu yake ni katika lile ziwa ndugu yangu maadamu upo hai ebu tengeneza leo Mungu, anakupenda ndo maana amekupa wasaa kusoma ujumbe huu,sio wote wamepata nafasi kama yako ila wewe umepata basi usishupaze shingo tengeneza sasa naye atakusamehe na kukurehemu..
May be an image of 2 people and sculpture

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA