JINSI TABIA ZINAVYOWEZA KUKUHARIBIA NDOA YAKO/MAHUSIANO

 Kuna nyakati unaweza ukawa unalalamika kwanini Mume/Mke wako amepunguza mashamsham ya Mapenzi au ukimpata Mwanaume/Mwanamke anakuacha kwenye atua za awali za uchumba, au ndoa yako inateteleka, kumbe tatizo ni tabia zako ndizo zinakukosesha baraka zako.

.
.
✍️Mwanandoa ambaye hampi Mume /Mke wake nafasi ya kupumua, muda wote anataka pesa, story zake "Ninunulie hiki, nataka kile".
Hawa huwa chukizo kwenye NDOA, na endapo atakuwa nae basi ni kwaajili ya tamaa za kimwili tu, au alimpenda sana Mume/Mke wake kiasi kwamba anashindwa kumuacha, lakini bado moyoni anakuwa anasononeka juu ya huyu Mume/Mke wake
.
✍️Wapo anayejifanya ana nguvu ya kutawala, yeye ndio kichwa, Mume wake ndio mkia.
Huwa hana heshima, hana utiifu, hana adabu kwa Mumewe.
Mwanaume yeyote mwenye akili timamu huwa anachukia kutawaliwa, hivyo Mwanamke alie mbabe, mpenda kutawala, huwa ni chukizo kwake.
.
✍️Usaliti huwa haupendwi na Binadamu yeyote yule, hata yule anaye saliti huwa hapendwi kusalitiwa. Waaminifu huwa wanachukia wenza wasaliti, lakini pia huwa hawana ndoto ya kufunga Ndoa Mwanaume/Mwanamke mwenye tabia za huruma(yeyote anayetaka anampa).
.
✍️Hawa ni Wanandoa wa Kike ambao kelele muda wote, hawapitwi na kitu "Yuko tayari aache mtoto ndani/asimpikie Mume wake sababu ya sherehe za mialiko aliyoipata", Kila kona anajulikana yeye, ana mazoea mabaya na wanaume wengine,
✍️ Mwanandoa anaye jifanya anajua kuliko Mume/Mke wake .Mume/Mke wake akisema hivi au vile , Yeye anamuona hajui na maneno ya kejeli/dharau anayatoa.
Kila kitu anataka asikilizwe yeye tu, Mume /Mke wake atakalosema/shauri linaonekana halina kichwa wala miguu.
Haambiliki, mkurupukaji, kila kitu "Niache ", hashauriki.
.
✍️Wapo Wanandoa wa Kike ambao anachoona fulani kafanyiwa na yeye anataka bila hata kujali uwezo wa Mwanaume wake. Rafiki yake kapelekwa shopping na yeye anataka, wakati huo Mwanaume hana hata uwezo wa shopping .
.
✍️Ni aina ya Wanandoa ambao wao hawaachi jambo likapita, watalitunza na endapo utafanya kosa basi litatumika kukuadhibu. Ukifanya kosa leo, litachukuliwa kosa la mwaka Jana ,Juzi , yote yataingizwa. Muda mwingine bila hata kufanya kosa, unaweza jikuta akalikumbushia na kuanza malumbano tena upya.
.
✍️ Mwanandoa ambaye anapenda kumlinganisha Mume/Mke wake na Boyfriend/Girlfriend wake wa zamani, kama anawajua Wapenzi wako wa zaman basi hata mkigombana kidogo lazima atayataja majina yao.
Anapenda kukuhukumu kuendana na historia yako ya nyuma .
.
✍️ Hii ya Mwanandoa ambaye analinda usalama wa Mume/Mke wake mpaka inageuka kuwa kero.
Wivu ndio Mapenzi, lakin huyu ana wivu kupitiliza, atapekua simu ya Mume/Mke wake au atapenda kumfuata nyuma nyuma, kufatilia kila mahali na akimkuta ni varangati muda wote, atapenda kuuliza "Huyu nani, kwanini ulikua unaongea na flani", ugomvi ndani kila saa, kuhojiana kila wakati.
.
✍️Mume/Mke ambaye jambo dogo kanuna, mara kakasirika, kidogo ugomvi.
Hataki ndugu, hataki wazazi, hataki wafanyakazi, anataka muda wote awe yeye tu.
.
✍️ Hawa wachoyo, ndo huwa tatizo zaidi.
Mfano: Ndugu wakija watashindia maembe, lakini yeye atakula na kufurahi kivyake.
Huwa anajiwazia yeye tu, vyake tu, hawazii wengine, vyake huwa vyake na vyako huwa vyake pia.
.
✍️Mume /Mke 👈Huyu huwa ni mtihani, mchafu muda wote, hajitambui wala kujitunza. Uchafu huwa ni kero kwa Mume/Mke wake.
.
✍️Mume/Mke ambaye hana kifua, Kila jambo/mipango/siri za ndani ya ndoa yake/mahusiano yake lazima ataitoa.
Hachelewi kumtangaza Mumewe kama ana kibamia, hana hela, kafanya hivi mumewe. Au kusema Mke wake ni bwawa la samaki wa kufungwa
Akikosana na Mume/Mke wake basi marafiki, ndugu, wazazi, majirani, wote watajua kama amegombana na Mume/Mke wake kwasababu fulani.
Haya jichunguze wewe Una tabia gani 🙄❓na uanze kubadilika.
Aidha ili uilinde Ndoa yako, au kama hujaolewa/kuoa bado basi ili upate wa Mwenza atakaye vutiwa na tabia zako.
UJUMBE UMEFIKA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA