MWANAUME!! HIZI NDIZO SIFA ZA MWANAMKE ANAYEFAA KUOA

 Mwanamke unachohitaji ni Mwanaume mwenye kujua thamani na utu wako, ambaye ataufanya moyo wako uwe ni moyo wenye amani na furaha kila Wakati na si kuhadaika na mifuko yake.

Unaweza kuvaa Pete ya NDOA leo na kesho ukatamani uivue, unaweza kufunga NDOA leo lakini kesho ukatamani bora ulivyokuwa SINGLE.
NDOA ni safari mpya katika maisha yako, na kumbuka tabasamu zote uzionazo kwa mabibi harusi siku ya NDOA zao, mara nyingi huwa MACHOZI ya baadae.
Take care, mtegemee MUNGU akupe MUME bora na kabla hujamuitaji MUME bora basi wewe kuwa MWANAMKE bora kwanza.
Mwanaume au Mwanamke anaeyakubali mapungufu yako na kuzivumilia changamoto zako, huyo ni bora katika maisha yako, kwasababu yeye ni zaidi ya furaha na amani unayoihitaji.
Kamwe usiache kumpenda, kwani hiyo ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo wengi wanaililia kuwa nayo.
Usisubiri kuiyona THAMANI ya MUMEO au MKEO pale anapoondoka kwenye himaya yako, badala yake ijue THAMANI yake leo, maana leo ndio nafasi yako kwake.
Anza kufanya hivyo leo, kesho huwezi jua itakuwaje, itumie vizuri nafasi aliyokupa na muda aliokupa ili kuiyonyesha thamani yake ndani ya moyo wako.
Usitabasamu wala kufurahia pale inapotokea au anapotokea MWANAUME kukuambia kuwa angependa kukuoa, yaani kufunga nawe NDOA.
Badala yake jitafakari na ujiuliza maswali zaidi ya miamoja juu ya maisha ya NDOA hiyo, kisha piga goti na kumuomba MUNGU ili MWANAUME huyo akawe kiongozi wa NDOA na maisha yako.
Baadhi ya sifa za Mke mwema,
1: Awe mwenye tabia njema.
2: Awe mwenye kuishika dini.
3: Awe mwenye heshima na adabu.
4: Awe mwenye kuvaa kwa staha na heshima.
5: Awe mwenye kuwapenda na kuwaheshimu wazazi wako na wake.
6: Awe mwenye mapenzi ya dhati na anayejua kupenda.
7: Awe mwenye kauli njema na za adabu.
8: Awe mwenye malengo na mtazamo wa kimaendeleo.
9: Asiwe mtu wa makundi sana na starehe.
10: Asiyependa kuiga.
11. Asojivunia uzuri wake.
12: Awe mwenye kukusikiliza na kukutii.
13: Awe msafi wa mwili, nguo na tabia.
14: Asiwe mtu wa ugomvi na mwisho,
15: Awe Mchapa kazi
May be an image of 1 person and handbag

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA