ZIJUE AINA 7 ZA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

 





Wanasaikolojia mbalimbali wamejaribu kuelezea aina za mahusiano ya kimapenzi ambayo wapenzi wawili wanaweza kuwa wanayapitia katika kipindi flani cha mahusiano yao.


Lakini kabla hatujaangalia hizi aina lazima tujue kuna vitu vitatu vinavounda na kudetermine ni aina gani ya mahusiano ya kimapenz watu wako nayo kwa mda huo.

Kuna kitu kinaitwa TRIANGULAR THEORY OF LOVE yaani Intimacy, Commitment na mwisho kabisa ni Passion. Nitajaribu kuelezea kwa ufupi kila kimoja kabla sijaingia kwenye point ya msingi yenyewe.

Intimacy

Hii ni hali ya kuwa karibu kihisia na mpenzi wako. Kuna hali flani hivi hutokea yaani unakuta mnashare the same feelings. Sijui kama ishakutokea unataka tu kumpigia simu mpenzi wako ghafla unakuta naye anakupigia. Nafsi zenu zinakuwa zinaongea na unajikuta unachowaza wewe ni sawa cha mwenzi wako.

Commitment

Hali ya mtu kuhakikisha uhusiano na mpenzi wake unabaki salama hata iweje. Mtu hapa anaweza kuwa katika uhusiano lakini asiwe committed kwa lolote kuhakikisha uhusiano unadumu kwa mda mrefu. Yupo na anakupenda lakini ikatokea chochote mkaachana yeye anaona sawa tu.

Passion

Hiki ni kitu kinachoweza kukusukuma uwe katika hali ya kimahaba na mpenzi wako. Muonekano wako kimwili inaweza kuwa macho mazuri kwa mwanamke, wengine makalio nk au unakuta kifua kizuri au muonekano maridadi kwa mwanamme.

Baada ya kuangalia hayo tuingie sasa katika aina za mahusiano ya kimapenz na hizi aina zinategemea kwa kiasi kikubwa hizo three components. Yaani intimacy, commitment na passion.

1. CONSUMATE LOVE

Hi ni aina ya mahusiano ya kimapenzi ambapo kuna zote hizo components tatu yaani intimacy, commitment na passion. Na kujua kama mko katika aina hii ni pale mnapoweza kufurahia sex or any physical affection, kila mtu yuko committed kuhakikisha mnafika mbali mna mda mzuri wa kuwasiliana, kila mtu anaweza kushow ni kitu gani kinamvutia toka kwa mpenzi wake na kuonesha positive response. Kiujumla hii ndo daraja la juu kabisa katika aina za mahusiano ya kimapenzi.

2. COMPANIONATE LOVE

Hii inahusisha two components yaani Intimacy na Commitment. Utaona hapa Passion hamna na aina hii hutokea sana kwa wale marafiki wa karibu mno na mwisho hujikuta wanakuwa na Malengo yao ya mbali na inaweza kuwa kuoana.

Mtu yuko ktk mahusiano unamuuliza umempendea nini huyo unakuta hana cha kukueleza zaidi atakuambia nampenda tu. Hapa mtu haangalii physical attractions zozote zile lakini yuko committed kuhakikisha wanaishi pamoja muda wote na anampenda sana. Utakuta mwanamke ana sura mbaya au mwanaume yupoyupo tu ila kutokana na kuwa karibu kwa muda mrefu wanajikuta wako katika mahusiano.

3. EMPTY LOVE

Hakuna Intimacy na Passion, kuna commitment tu. Unaishi na mtu huna hisia naye hata kidogo wala hata sexual attractions zozote kwake huzioni zaidi unachowaza ni kuishi nae tu. Hakuna kujuliana hali na inaweza pita hata siku au wiki hata huoti chochote wala kumwaza mpenzi wako.

Na hii hutokea sana kwa wanandoa, unakuta baba anachojua ni kuacha hela ya mboga mezani tu na akirudi hata wazo na wewe hana na hata upande wa mwanamke anachojua ni kumpikia mumewe kama wajibu wake na kuweka mezan kisha kuendelea na shughuli zake.No intimacy no passion.

4. ROMANTIC LOVE

Katika hii aina tunaona kuna Intimacy na Passion tu, hakuna commitment. Hapa kuna kushare vitu vingi sana na mahaba yenye hisia kali sana sema huwa hayana mipango mirefu au hayadumu sana sababu there is no commitment. Na haya huwa hayafiki mbali sana.

5. INFATUATION

Hapa kuna Passion tu, no intimacy wala commitment. Infatuation ni Ile hali ya kuvutiwa na mtu flani kimapenzi kutokana hasa na physical attractions.

Mfano unaweza mwona mwanamke may be ana shape kali tayari ukawa umevutiwa naye hiyo tunasema infatuation na haiwezi kuwa LOVE coz kuna possibility kile kitu ulichovutiwa nacho kikapotea na hutamtaka tena. Na hii huwa haidumu sana sababu physical attractions may change according to the environment. Umemwona mwanamke au mwanaume anapendeza we ukamrukia mwisho akibadilika lazima umkimbie tu sababu kilichowaunganisha pale ni physical attractions na sio vingine yaani no intimacy no commitment.

6. FRIENDSHIP LOVE

Hapa kuna intimacy tu bila passion wala commitment katika maana ya kimahaba. Mnakuwa mnapatana ama kuelewana sana na nafsi zenu ziko kwenye mstari mmoja lakini hamvutiwi kimwili.

Mara nyingi huweza kuwa mzizi wa aina nyingine za mapenzi.

7. FATUOUS LOVE

Katika aina hii ya mapenzi kuna commitment na passion lakini intimacy/liking inakuwa hakuna. Mara nyingi hii hupelekea uchumba wa ghafla ukifuatiwa na ndoa ambapo passion inakuwa imechagiza commitment kabla ya kujenga msingi wa intimacy.

Mara nyingi ndoa za hivi hazidumu au huwa na misukosuko pale passion inapofifia(kuonana kawaida) na kupelekea migogoro inayotokana na kukosa msingi wa urafiki(intimacy)

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA