Nachokaga mimi why washauri wakubwa sana kwenye mahusiano wengi sana wako single
Makungwi nao
1. Hapo zamani nilikutana na mtu aliyeniambia kwamba kusema ukweli utakaomfanya mtu alie, ni bora kuliko kusema uongo utakaomfanya atabasamu na kufurahi.
2. Akaniambia kuwa marafiki zangu wa kweli ni wale ambao hawatonikimbia baada ya kupata marafiki wapya.
3. Aliendelea kuniambia kwamba iwapo watu hawatambui na kuthamini uwepo wangu, natakiwa kuchapa kazi ili wathamini na kutambua umuhimu wangu pale watakaponikosa.
4. Alisema sipaswi kumkasirikia mtu ambaye amenikalia kimya kwa sababu lazima kutakuwa na sababu ya yeye kukaa kimya, na kwamba sababu hiyo nitaijua baadae.
5. Aliniambia daima ni heri kuwa baraka kwa wengine muda wote kuliko kuwa mzigo muda wote.
6. Akasema lazima nijue kuwasamehe wengine sio kwa sababu wanastahiki msamaha bali kwa sababu ninastahiki kupata amani inayotokana na msamaha.
7. Natakiwa kujua kuwa kila mtu anastahiki kupewa nafasi nyingine na nafasi nyingi zaidi kama akiomba msamaha, lakini sipaswi kuacha kujilinda dhidi ya dhamira na nia yake.
8. Sipaswi kuongea na watu pale tu ninapokuwa na muda, bali natakiwa kutengeneza muda wa kuongea na watu.
9. Natakiwa kujua kwamba huwenda ukweli ukaniumiza kwa muda mfupi, lakini uongo utaniumiza kwa muda mrefu.
10. Natakiwa kuwathamini na kuwaheshimu watu wanaosema ukweli bila kujali ukweli huo unauma kiasi gani.
11. Natakiwa kufanya maamuzi ninapokuwa katika hali maridhawa, sio ninapokuwa na hasira. Vivyo hivyo sitakiwi kutoa ahadi ninapokuwa na mizuka ya furaha.
12. Natakiwa kutambua kuwa baadhi ya watu ni kama mishumaa inayojichoma ili kuwaangazia wengine. Sitakiwi kujutia ikitokea nikawa mmoja wa mishumaa hiyo.
13. Natakiwa kujifunza kuwa rafiki maridhawa kwa sababu ni bora mara elfu kushinda mpenzi asiyejali.
14. Natakiwa kuyathamini na kuyalinda mahusiano yangu ya miaka mingi ya uwekezaji kwa sababu mahusiano hayo ni kama kitabu ambacho hukuchukua miaka mingi kukiandika lakini kinaweza kuungua ndani ya sekunde chache tu.
15. Alinisisitizia kwamba iwapo nina tatizo na mtu basi natakiwa nimwambie mtu huyo badala ya kwenda kuitangazia dunia kwamba nina tatizo na mtu fulani.
16. Akaniambia natakiwa kutambua kuwa hakuna mtu ambaye yuko "bize" kupita kiwango, bali unatakiwa kujua wewe uko nafasi ya ngapi kwenye maisha yake.
17. Akaniambia kuwa watu wanaweza kukuamini pale unapokuwa na msimamo na kile unachokisema na unachokifanya.
18. Akaniambia kwa sauti ya chini: "Mungu pekee ndiye anaweza kuaminika. Muamini Mungu kwa asilimia 100".
19. Kisha akasema, kwa vyovyote vile nisiwasahau wale walionisaidia na wakasimama nami katika nyakati za shida na nyakati ngumu za majaribu.
20. Daima natakiwa niwakumbuke wale walionitenga wakati wa matatizo yangu. Sio kwa ajili ya kisasi, bali kama funzo kwangu katika maisha.
21. Natakiwa kuwa mwangalifu na wale walionitumbukiza kwenye matatizo lakini nisiwachukie. Kwani hilo ni funzo la maisha.
22. Tena akaniambia daima natakiwa kumshukuru Mungu kwa maisha na uhai alionijaalia. Amenipendelea, sio haki yangu.
23. Wakati akiondoka aliniusia nikumbuke kuwa maisha haya ni mapito tu, daima natakiwa kutambua ukweli kwamba kuna maisha baada ya haya
24. Alitabasamu na kuondoka huku akiendelea kunipungia mkono hata alipofika mbali. Je, mtu huyu ni nani?
25. Aliyoniambia yanaweza kukufaa, kama ni hivyo basi shea na wengine.
Mungu azidi kukubariki wakati ukiendelea kuyatafakari maneno haya.