UKISHA OLEWA JIANDAE KUMWAMINI MUMEO
Sometimes ngumu sana kumuelewesha mwanamke jambo flani, iwe kuchelewa kurudi, sms/calls za wanawake and the like
Wanawake mjifunze kuwaamini waume zenu.
Kuna wakati Mme wako anaweza kuchelewa sana kurudi nyumbani na akakupa sababu ambayo huwezi kamwe kuiona kwenye kitabu chochote duniani.
Ruhusu upendo na uaminifu vitamalaki.
Fikiria Yona anarudi nyumbani baada ya siku 3 tangu ameondoka, hakupiga simu, hakutuma ujumbe, wala chochote, ila tu akamwambia mkewe kuwa alimezwa na samaki na kutapikwa baada ya siku 3 - hebu tafakari hilo.
Mke wa sasa anaweza na anataka ampasue hata kichwa.
''Ulimezwa na samaki? Hivi unadhani unaongea na mtoto?
Dharau gani hiyo, kunidanganya mie kama sina ubongo? Samaki gani huyo? Sangara au Sato?
Hata kama Yona angemweleza hayo paroko/mchungaji/shehe ni lazima angemwita faragha na kumwambia:-
"kaka Yona kwa nini usisali na kutubu kuhusu dhambi za uongo?".
Majirani wangesema, "mwanamke mwenzetu ujue samaki huyo ni Mwanamke mwenzio tu"
Lakini kati yangu na wewe, tunajua ni kweli Yona alisema ukweli.
basi wanaume waaminiwe tu jamani.
,
Najua hata hii hamtaamini