AMENIACHIA WATOTO WAKE NA KUONDOKA SIJUI YUKO WAPI?
Nilikutana na huyu Kaka mwaka jana, aliniambia kuwa ameoa lakini mwanamke anamsumbua sana, mimi nilimpenda kwani alionekana mstaarabu, tulianzisha mahusiano na kweli mwanamke wake ni msumbufu sana, ni wale watu wakupiga simu kumi si kidogo na akipiga anamtukana mwanaume kama mtoto, hajishughulishi kwa chochote yeye ni kuomba pesa.
Mwanaume alimchoka na kuamua kumuacha, kwakua mimi nina nyumba kubwa ya kazini basi alihamia kwangu. Tumeishi kama mke na mume kwa miezi nane, mkewe bado alikua akisumbua akiwatumia watoto kujaribu kumchukua mwanaume wangu kwani mwanaume alikua hamtaki tatizo lilikua ni ndoa ya kanisani mabyo ni ngumu kuvunja.
Mwanaume alipohamia kwangu mwanamke alivyo na roho mbaya aliondoka na kuwatelekeza watoto wake wa kuwazaa eti kisa mwanaume hahudumii wakati nilimuona alikua anajtahidi ila mwanamke ni kukaa tu. Nilimuambia yule kaka asijali, akawachukua wanae watatu na tukaja kuishi nao, nimeishi nao kwa miezi miwili lakini ghafla mwanaume akabadilika.
Mkataba kazini kwao uliisha akawa anakaa tu nyumbani hajishughulishi. Nikimuambia anakua mkali, sasa wiki iliyopita nimerudi kutoka kazini mwanaume kaondoka bila hata kuniaga, nimejaribu kumpigia simu alikua hapokei, jana ndiyo akanitumia meseji akaniambia yeye kaenda kutafuta maisha nikae na wanae akipata atakuja kuwachukua.
Baada ya hapo simu yake haikupatikana tena, nimejaribu kumtafuta kila mahali lakini hapatikani. Kibaya zaidi sijui hata ndugu zake, baadhi ya marafiki zake ninao wafahamu wananiambia kuwa anatokea Mwanza lakini hata hawamjui.
Mwanamke wake naye ni mtu wa Kigoma na alishaondoka na sijui hata alielekea wapi. Niko njia panda mwanaume kanitelekezea watoto wake watatu nawaza niwapi pakuwapeleka, hata hatujafunga ndoa lakini ananiachia majukumu nashindwa niwafanye nini hawa watoto.