UKWELI KUHUSU WANAWAKE

 

💞1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema. Maombi Hufungua Vingi Kuliko Mapenzi Kufungua Miguu Tuu.
💞2. Mwanamme bora KAMWE hapimwi kwa İdadi ya wanawake alionao au
aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia "Mimi ni mume wa mtu" au "ninae mtu tayari."
💞3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama
yoyote ile, wanawake wanaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kulika tabia zao"
💞4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo ake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Atathamini mali za mumewe! Usimwache Ndie Mke Bora.
💞5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza
💞6. Tafuta mwanamke ambae atakupa challenge ya maisha na kuongeza
uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee
💞7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.
💞8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza, Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu
💞9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio kuvaa hereni kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba hiyo haifai.
💞10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku tu, ila Pia tumia kichwa chako kuwaza
mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa.

1. Mwanamke anapokasirika, zaidi ya nusu ya mambo anayoongea anakuwa hajamaanisha.
2. Wakati mgumu kabisa kwa mwanamke ni pale anapokuwa mbali na mwanaume anayempenda kwa dhati au anapogundua kuwa mumewe ana mahusiano na mwanamke mwingine.
3: Mwanamke sio kama "tangazo la OMO" usipomfurahisha na kumtunza... wengine wataifanya hiyo kazi badala yako.
4. Inamchukua muda mwanamke kumuamini mwanaume, na akikuamini ni ngumu kumbadilisha, lakini ukijichanganya, sahau kabisa kama atakuamini tena.
5. Mwanamke ni shule ambayo huwezi kuhitimu.
6. Cheti unachopewa unapomuoa mwanamke sio "leseni ya udereva" bali ni kama "kibali cha mwanafunzi".
7. Anaweza kuwa mchungu sasa hivi, lakini baadaye akawa malaika mtamu.. Itategemea namna utakavyoishi naye.
8. Ni ngumu mwanamke kusahau vitu, anakumbuka zaidi yale yanayomuumiza zaidi, hivyo epuka kumuumiza.
9. Mwanamke anaweza kuwa msiri sana... muda mwingi anapokwazwa na jambo anaenda kwa mtu wake wa karibu, analia.
10. Wanawake wote wanapenda kuombwa. Mara nyingi wanaume wanalisahau hili.
11. Wanawake wote wana tabia ya kipekee kama chumvi, unaweza usitambue uwepo wake lakini akikosekana vitu vyote vinakosa ladha.
12. Akikupenda kwa dhati anaweza kufanya chochote unachotaka afanye madamu kinakufurahisha, hivyo usimlazimishe kukupenda.
13. Mkeo anaekupenda kwa dhati, hata kukuomba pesa ataona aibu, na hasa kama anakupenda hawezi kuvumilia matumizi yako mabovu ya pesa... hayo ni miongoni mwa mambo yanayowafanya wanawake kuwa viumbe maalum kabisa..

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA