MWANAMKE TUMIA VIUNGO VYAKO KUNOGESHA PENZI SIYO KUHARIBU MAPENZI


*Regeza jicho wakati wa kumtizama mume wako siyo unalikaza mpaka anakuogopa utafikiri uko chooni unakamua kimba lililokataa kuoka😂😂😂😂😂*
Usiseme nina pua baya sijui nini,
mwanamke ukiongea na mumeo hata kama unapua kama nukta nundu shikashika huku ukijifanya kama unamafua vile.
Hata kama unasikio kama ungo lipambe kwa hereni siyo lazima za kuning'inia kama mmasai,
zipo ndogo akija mume ataliona sikio dogo unakwama wapi mwanamke?
Hakuna limbwata zuri kama nywale lakini mmh,
kuna baadhi ya watu nywele zimefungwa mabutu wala hazijulikani rangi wala mstari hauonekani.
Wanaume wengine wanapenda kuchezea nywele jamani suka vizuri ata twende kilioni😂😂😂😂,
Mume mpaka kula denda anaogopa kwa meno yalivyogandia vinyuzi vya spinachi na maharage😂😂😂😂
Mswaki unaona kama gundi ya viatu,
halafu unasumbua watu mume wangu wala hani kiss, mara naombeni jinsi ya kutengeneza limbwata,
wakati wewe mwenyewe limbwata hala hujui kujituma
Mwanamke una kauli chafu kama choo cha stendi ya ubungo,
mume anaona bora arudi nyumbani saa 5 au 6 kawahi saa 4
Na bado atarudi mpaka asubuhi kama hujajielewa na kauli zako,
Mwanamke poda toka umepambwa siku ya harusi mpaka leo hata wanja huujui,
utamsikia mimi poda inanitoa vipele,
wanja na lipstik jee zinakutoa vidonda na majipu?
Jamani siyo lazima cheni lifike tumboni vaa hata fupi jiongeze,
Mwanamke mkono wako usiishe hina na vaa saa na cheni za mkono, utamsikia mwanamke anasema mimi siyo muhindi nikitembea kama nimejifunga mabati 😂😂😂😂wengine waume zao wanajitahidi kwa mapambo kuwanunulia lakini wavaaji sasa hawapo au yanawekwa kabatini ni kwa ajili ya harusi tu.
Usieneze pete midole yote vaa japo 1 ili mume naye akikushika mkono aone tofauti.
Huwezi kuvaa shanga vaa cheni siyo kiuno kipo plain kama cha mwanaume.😂😂😂😂🙈🙈
May be an image of 1 person and standing

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA