KUJITUNZA KWA MWANAMKE NDIKO KUNAMPA THAMANI YA KUPATA MUME MWENYE HEKIMA
Kwanza nianze na ;-
HEKIMA YA MWANAUME.
Heshima ya Mwanamke ndiyo humbadili Mwanaume na kujiweka katika usawa wa tabia halisi ya Mkewe
Mwanamke anayo nguvu kumbadilisha Mwanaume na kumpeleka kwenye HEKIMA
Mwanamke akiwa Mama Mwema anakuwa Mwalimu wa Mtoto/watoto na uzao wake unarudisha heshima kwenye maisha yake ya uzeeni, ndivyo itakavyokuwa kwa Mwanamke akiwa mke mwema huwa nguvu ya Mumewe na Mume wake humtunza mkewe
Mpaka hapo unaiona maana halisi ya Mwanamke kujitunza ili anapoianza safari ya maisha yake ajiweke huru kwa Mwanaume mmoja ambaye atampa heshima ya kuitwa MKE
Aina ya ndoa za sasa zimetawaliwa na MALIPIZI YA MAHUSIANO kila mmoja kutafuta namna ya kumuumiza x wake, ndo maana unakuta ndoa za sasa zinaleta FURAHA NA AMANI kipindi cha mwanzo tu na wakiisha kaa mwezi mmoja kila mmoja anaanza kumtafuta x wake ili amfariji kwani ndani kunawaka moto
Wanaume kwa uhalisia wao wanaendeshwa na Mwanamke ki tabia ikiwa tu:-
MWANAMKE ANAYO NGUVU NDANI YA MWANAUME
Sio kila Mwanamke anaweza kuwa na nguvu kwa Mwanaume, na hilo linasababishwa na HULKA YA KIUMENI kutamani kila Mwanamke anayekuwa mpya machoni
HITIMISHO :-
TABIA NJEMA YA MWANAMKE NDIYO HUITENGENEZA AKILI YA MWANAUME
Uzuri ama muonekano wa Mwanamke haumfanyi Mwanaume kuwa na HEKIMA maana Mwanaume huona fahari kuwa na MKE MWEMA
Mwanamke kuwa Mke mwema Kuna vigezo na sio kila Mwanamke anaweza kupata kibali hicho bali Kuna UPENDELEO MWANAMKE KUWA MKE MWEMA.
#Elista_kasema_ila_sio_Sheria