HII INAWEZA KUWA NDIYO SABABU KILA SIKU MNAGOMBANA!

Photo by IDDI MAKENGO🇹🇿 on September 14, 2020. Image may contain: 1 person, closeup.

Ndoa nyingi zinavunjika si kwasababu wanaume ni wakatili, si kwasababu ndugu wameingilia, si kwasababu mwanamke ni mchoyo au hajui kumjali mume wake bali kwakua wanandoa wenyewe hawajuani. Wakati mwingine wanandoa wanaweza kuwa wanataka kitu kimoja lakini namna ya kukiendea hicho kitu ikafanya wagombane na hata kusababisha kuvunjika kwa ndoa.

Naomba nikupe mfano rahisi tu, kwamfano mke anakerwa na tabia ya mumewe ya kuchelewa kurudi nyumbani, kila siku mke analalamika na kulia, inafikia hatua ya kuwaambia ndugu na hata wakwe zake. Lakini mume nayeye anatamani kurudi nyumbani, amkute mkewe ana raha, wale chakula vizuri bila kelele. Anachukia pale mkewe anapoanza kelele za kwanini umechelewa.

Anakereka pale mke anapopiga kelele kwa ndugu na marafiki, hii humfanya kuchelewa kurudi si kwasababu anapenda au kuna kitu cha maana anachokifanya huko mtaani!

Hapana anachelewa ili kukwepa kelele za mkewe. Hapa utaona wote wanataka kitu kimoja, kuwahi nyumbani na ndoa kuwa na amani. Lakini wote wanagombana kwakua hakuna anayejua mwenzake kwanini yuko hivyo. Mke hajui kwanini mume anachelewa na mume hajui kwanini mke anapiga kelele. Mke hapendi mume achelewe mume hapendi kusikia kelele kila siku hivyo mume anachelewa na mke anaendelea kupiga kelele.

Ndiyo kuna matatizo mengi sana kwenye ndoa ambayo ungeweza kuyasuluhisha kama ungemjua mwenza wako. Mwanaume jua saikolijia ya mkeo na mwanamke jua asikolojia ya mumeo, kwisha habari mtaishi kwa amani. Sasa huu ni mfano mmoja, kama bado hujasoma kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” nakuambia tafuta Elfu kumi tu utajifunza mengi, kitabu unaweza kukipata ndani ya dakika tano, kwanjia ya E-mail, Whatsapp au hapahapa Facebook.

Inawezekana hujaoa au hujaolewa, unaweza kujifunza pia, lakini ndoa yako inafuraha, sasa kwanini usubiri mpaka ivunjike ndiyo uanze kulia na kuomba ushauri, kwanini uendelee kugombana na mwenza wako kila siku. Lipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa 0657-552-222 kisha tuma meseji humu Facebook au kwenye namba 0742-381-155 kusema unataka utumiwe kitabu kwa njia gani.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA