NJIAPANDA; NIFANYE NINI WIVU WA MWANANGU UMENIFANYA KUPEWA TALAKA?





Mimi ni Mama wa watoto wawili, nimeolewa na ndoa yangu ina miaka miwili sasa. Mimi na mume wangu tuko vizuri,a naanihudumia na hakuna shida yoyote, mtoto wangu wa kwanza nilizaa na mwanaume mwingine ambaye tulishindwana na kuachana, yeye akaenda kua mwanamke mwingine na mimi nikaolewa, Baba wa mtoto anahudumia vizuri mtoto wake na kila likizo anaenda kukaa kwake.

Sababu ya kuja kwako ni hivi, mwanangu nahisi kumpoteza, mke wake ni mtu mzuri sana kwa mwanangu. Mwanangu ana miaka mitano, lakini kila akirudi kutoka likizo kwa Baba yake anakua na furaha na anatamani kubaki huko huko. Najaribu kumchunguza kama Mama yake wa kambo anamtesa lakini wapi, anaonekana anampenda.

Naumia sana, mwanzo nilikua naumia na picha ambazo alikua anapest Baba yake. Labda mwanangu ameenda wametoka wote na mkewe, wanacheza, mtoto wangu anaonekana kuwa na furaha akiwa na yule Mama kuliko hata mimi. Hali hiyo ilikua inaniumiza sana kwani naona kama wana raha kuliko mimi.

Baaada ya kuumia sana nikaona ili wasiwe na raha basi nimgombanishe mke wake na mwanangu kwakua baba yake anampenda mtoto basi watachana. Nilianza kumlazimisha mtoto awe anaongea kwa Baba yake kuwa hataki kwenda kwaku Mama anmnyima chakula na kumpiga. Alikua anaongea kwa lazima nikiwa namuangalia, mwaka jana niligoma kabisa kuwa mtoto asiende kwa Baba yake kwakua Mama yake wa kambo anamnyanyasa.

Ilizua ugomvi mkubwa sana lakini nilisimamia msimamo wangu, tukaenda mpaka ustawi wa jamii mwisho ikaamuliwa kuwa Baba wa mtoto awe anakuja kumuona mtoto kwangu lakini si mtoto kwenda huko. Hapo nilikua na amani kidogo kwani mwanangu alikua haonani tena na yule mwanamke. Baba yake akawa anakuja Morogoro kwani wao wanaishi Dar, anapanga chumba nampelekea mtoto anakaa naye sikumbili anamrudisha.

Lakini Kaka bado sikua na amani kwani niliona wana furaha wanapostiana, nilidhani labda kwakua mke wake hampendi mtoto wake basi watagombana, nilijikuta nakua na kisirani mara kwa mara mpaka mume wangu naye tukawa tunagombana ingawa alikua hajui sababu ya ugomvi.

Baada ya kuona kuwa hawagombani basi nilianza kumpigia simu mwanaume usiku kumuomba matumizi ya mtoto.

Nilikua navizia mume wangu kalala, nachukua simu nampigia usiku kumuambia labda mtoto anaumwa, namuamsha mtoto usiku wa manene namuambia aongee na Baba yake lengo likiwa ni kumkera huyo mwanamke ili aongee kitu kuhusu mwanangu. Nilipoona hakuna kitu nikaanza kumpigia simu huyo mwanamke, usiku namuambia kuwa simpati mume wake nahitaji kuongea na Baba wa mtoto wangu.

Basi alichokua anafanya ni kumuamsha mume wake na kumpa simu bila kulalamika au kusema chochote. Wakati nafanya hivyo sikujua kama mume wangu alikua anaifuatilia. Kumbe alikua anajua kuhusu simu za usiku, alishaongea na mtoto kama kweli alikua ananyanyasika na kuambiwa hapana. Hivyo juzi usiku wakati naongea na simu na Baba wa mtoto wangu mume wangu alinifuata chumbani kwa mtoto na kuniambia nikimaliza kuongea naye kesho yake nipaki vitu vyangu nimfuate.

Nilishtuka nikamuambia kuwa nilikua naongea naye mambo ya mtoto, akaniuliza mambo gani, kama mtoto anaumwa mbona sikumuamsha yeye naenda kumuamsha mtu ambaye yuko dar. Yeye mtoto wangu anamhudumia kwa kila kitu na hajawahi kumtenga. Nilikua sinajibu ndipo akaniambia kuwa, anaona kuwa bado nampenda X wngu hivyo hawezi kuishi na mimi kama kila siku naamka kwaajili ya kuongea na X wangu.

Anachojua mume wangu nikuwa, usiku napiga simu ili kuongea na X wangu kwakua bado tunamahusiano, pia anajua kuwa sababu ya kutotaka mtoto aende Dar ni mipango yangu ya mimi na Baba wa mtoto wangu ili tu tuonane Moprogoro akiaga kuwa anakuja kumuona mtoto0. Kaka si kweli, mimi simpendi X wangu, sina mpango naye, nampenda sana mume wangu lakini nilikua naona wivu tu namna alivyokua anaishi vizuri na mwanangu.

Nimejaribu kumuomba mume wangu msamaha lakinia kagoma, ameniandikia talaka moja na sasa hivi niko Eda. Kaka nisaidie nifanye nini ili mume wangu kujua ukweli kuwa nampenda na wivu tu ndiyo ulikua unanisumbua, nimeomba hata tuite wazazi lakini mume wangu anasema hataki kushirikisha mtu kwani wakati anataka kunioa hakushirikisha mtu. Kaka bado nampenda mume wangu lakini sijui ni namna gani nitamshawishi ili kuujua ukweli.
MWISHO

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA