JE MAHUSIANO YAKO HIVI??

Unapokuwa katika mahusiano ambayo unategemea yaishie katika Ndoa, huwa kuna Taa nyekundu ambazo huwaka kuashiria hali ya hatari kuhusiana na mtu uliyenae kwenye mahusiano.
.
Sikiliza kwa makini. Kama Mpenzi wako sio aina ya mtu ambaye unatamani uwe nae kwenye Ndoa, Basi Ndoa haiwezi kumbadilisha.
.
Kama kila siku ninyi ni ugomvi tu Jumatatu mpaka Jumatatu, Ndoa haiwezi kuwa-guarantee kuwa na masikilizano baada ya kuingia humo.
.
Watu wawili hawawezi kutembea pamoja wakaifurahia safari kama hakuna Mapatano. Upatano ni muhimu sana katika urafiki, mahusiano na Ndoa.
.
Kama mpenzi wako ni mtu wa kukuumiza kila iitwapo leo, mtu wa kukushusha thamani na kutokukuheshimu usije kufikiri labda Mkiingia kwenye Ndoa atabadilika.
.
Ndoa sio gereji ya kurekebisha tabia. Ndoa ni maisha ya uhalisia. Usiseme unampa muda wa kubadilika, ni vigumu kubadili tabia ya mtu mzima. MUNGU pekee ndiye anayeweza kumbadilisha mtu.
.
Mapenzi yasikupige upofu ukashindwa kuona Taa nyekundu. Wewe ni mtu mwenye thamani yako, sio mtu wa majaribio!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA