MATUNDA YA KAZI KULA NA MKEO ANAELIA NA WEWE MISIMU YOTE KUITAFUTIA FAMILIA BARAKA HAWARA HANA SHUKRANI.


Ni Mke wako pekee anaeweza kukuvumilia na kukupa moyo usipokuwa na Pesa,tena akakubali kulala na wewe kitanda kimoja akikutia moyo usiku kucha lakini siyo mchepuko.
Mchepuko anakupa mahaba ukiwa na kitu ila ukikosa anakwenda kwa mwingine,mkeo yeye jua liwake mvua inyeshe yupo nawewe,unaanzaje kumdhrau kama si kukosa akili?
Kwa hawara unaweza kuombwa pesa ya kidari na maini hata ukiwa mgonjwa mahututi akidai unaeumwa ni wewe na sio pesa lakini kwa mkeo ataenda hata kwao kuomba msaada akupikie maini ule upate nafuu.
Ni vema ukamheshimu mkeo!!
Mwanamke yeyote anaweza kukupa mwili wake ili uburudike kitandani lakini Mwanamke awezaye kukuhurumia kwenye maisha yako na kukuombea ukapokea BARAKA ni mkeo peke yake .
Hawara akikohoa tu unamuuliza umeniita baby,nguo za kila toleo anazipata toka kwako,lakini kwa mkeo hata chupi ya 500 hujui ni lini na wapi anapata,bajeti kwa mkeo ni pasua kichwa mpaka anapata homa za ghafla,ananyauka na kupauka tu,nyanya za masalo mtaani ni yeye anaulizwa mama fulani vipi leo huchukui halafu mwanaume unataka ubarikiwe?
Labda kwa baraka za shetani na sio Mungu Mwenyezi!
Ukirudi nyumbani unamuona mkeo mchafu,hana jipya,ananuka jasho,amekondeana bila kujua kwamba shamba lenye kutunzwa vizuri ndio inayotoa mazao bora.
Kuwa na akili ya kudumisha penzi na kulinda ndoa yako usichafue mikono na mwili ukaja leta magonjwa ya zinaa/ukimwi kwa mkeo na umasikini kwa familia.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA