#Kwenye mapenzi ukiona mtu anamsifia na kumuongelea vizuri sana mume au mke wake, haimaanishi kwamba huyo anayesifiwa ni mkamilifu au yuko perfect,

#Kwenye mapenzi ukiona mtu anamsifia na kumuongelea vizuri sana mume au mke wake, haimaanishi kwamba huyo anayesifiwa ni mkamilifu au yuko perfect, na kama ulidhania hivyo basi akili yako ina shida kidogo.
Iko hivi, kwenye mapenzi hatutafuti au kuishi na mtu mkamilifu bali mtu ambaye mazuri yake yanazidi maradufu madhaifu yake na yale madhaifu hayana nafasi kuathiri mtazamo wa huyu anayesifia.
Kwenye mapenzi tunatafuta anayebebeka na kuvumilika maana hayo ya kuvumilika kwake hayazidi yale yasiyovumilika, nasema hivi maana wapo ambao hawabebeki, hawachukuliki na hawavumiliki kwa jua wala kwa mvua.
Yamkini hawa ndio wale ambao huzitamani ndoa za wenzao, huwatamani wake na waume wa wenzao na hutokwa na povu sana wanapoona mtu anamsifia mpenzi wake.
Ndoa ni safari, hivyo jali safari yako.
```
Image may contain: 2 people, people standing and outdoor

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA