NAMNA YA KUOMBA USHAURI BILA KUPOTEZA UAMAUME WAKO!

Iddi Makengo - NILIDHANI KANIPELEKA KWAKE KUMBE NI KWA... | Facebook
Mwanaume ukitaka kudharaulika basi kuwa mtu wa kuendeshwa endeshwa. Kwamba huwezi kukaa na kupanga kitu na mwanamke wako bila kumshirikisha dada yako, Mama yako au kuomba ushauri kwa marafiki. Lakini kama unakaa na mke wako, mnapanga kitu lakini ukienda kuongea na Mama yko unarudi umebadilika basi jua mwanamke na hata hao wanaokupa ushauri lazima wakudharau kuwa huna msimamo.
Kuomba ushauri ni jambo la kawaida lakini ni lazima unappochukua ushauri wa mtu kama mwanaume uufanye kuwa wako ili uheshimike, basi hizo ndiyo mbinu za kuomba ushauri na bado ukabaki na heshima ya uanaume wako;
(1) Muambie kuwa ngoja nifikirie nitakujibu; Mko usiku, au mchana tu mmeongea, amekupa wazo, ni zuri au baya, lakini huna uhakika nalo. Ni lazima ukamuulize mtu, kuna rafiki, labda ndugu unamuamini sana mpaka umuulize. Badala ya kumuambia mwanamke, ngoja kwanza nikaongee na flani nimsikie anasemaje wewe muambie, subiri nifikirie nitakupa jibu. Usikubaliane tu na kitu kisha ukabadilisha mawazo au kusema unaenda kuomba suahuri, hapana, sema unafikiria, baadaye kaombe ushauri ukirudi muambie umekubali au umekataa, hayo sasa yatakua ni mawazi yako na atakuheshimu hata kama hatafurahi.
(2) Muambie nimeona ile kitu haiku sawa tufanye hivi; Ulishaongea na mwanamke, akakupa mawazo au mkachangia mawazo mkakubaliana, lakini unaenda wka watu wako wanakubadilisha, unaporudi kwa mwanamke, sema nimefikiria ile kitu hapana, naona tutakwama, nadhani tufanye hivi na vile na si kusema nimeongea na Mama ameseka hataki au nimeongea na rafiki. Hapo utaonekana umebadilisha mawazo wewe na hujabadilishwa mawaz0 na mtu hivyo heshima yako bado itabaki.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA