MWANAUME ANAAGA NA MWANAMKE ANAOMBA RUHUSA!


Photo by IDDI MAKENGO🇹🇿 on September 11, 2020. Image may contain: 1 person, standing, shoes and indoor.
“Kaka unasema kuwa mwanamke ukitaka kutoka hata kama hujaolewa ni lazima kumuambia mpenzi wako, kumuaga lakini mimi mpenzi wangu anatoka na marafiki zake haniagi ila nikitoka tu bila kumuga atalalamika mpaka basi nusu kuachana, hivi hii ni haki kweli?”

“Ni mara ngapi mpenzi wako alishawahi kuja kulala kwako?”
“Mara nyingi tu….”
Vipi asubuhi akiondoka unampa nauli ya kurudia kwake?”
“Hapana, utampaje mwanaume bnauli, yeye ndiyoa natakiwa kinipa?”
“Wewe ulishawahi kwenda kwake kulala?”
“Ndiyo….”
“Anakupa nauli?”

“Ndiyo, yeye si mwanaume anatakiwa anipe…”
“Yeye anakupa nauli lakini wewe humpi? Hivi hata siku moja ulishawahi kumsikia akilalamika kuwa akija wkako humpi nauli wakati yeye anakupa, sio haki sawa?”
“Hapana, sijawahi kumsikia akilalamika.”

“Basi Dada nadhani jibu unalo, kwenye mahusano mapak kwneye ndoa kuna mambo yakike na kiume, hakuna haki sawa kuna kila mtu kutimiza majukumu. Ukiolewa kama ukienda nyumbani kwenu kumshitakia mume wako kuwa hahudumii familia ataitwa kikao kuonywa kuwa huo sio uanaume, lakini kama utaenda useme kuwa mume wangu akityoka haombi ruhusa basi Mama yako atakurudisha yeye mwenyewe!

Katika ndoa mume anaaga na mke anaomba ruhusa, katika mahusiano mwanamke anaaga mwanaume anatoa taarifa. Ndiyo anapaswa kukuambia kuwa yuko wapi lakini si kukuomba ruhusa. Ni kweli ni raha ukijua lakini usishindane eti kwakua yeye hafanyi kitu flani na mimi sifanyi!”

MWISHO

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA