MWANAMKE USIJIFUNZE NDOA KWENYE MAHUSIANO

MAANA MAHUSIANO NI UWANJA WA ULAGHAI NA KUTUMIANA

Wanawake mnajikuta mnaangukia kwa wanaume mliowachagua wenyewe ila wao wanakuwa kwenu kwa sababu za ki MAPENZI

Kumjua Mwanaume mkweli ni jambo linaalohitaji utulivu wa fikra zako mwenyewe, Wanaume kwa maumbile yao TAMAA HUINULIWA NA MUONEKANO WA MWANAMKE HUSIKA na hapo ndipo neno NAKUPENDA hutamkwa, bila kujua chanzo cha Mwanaume kukutamkia NAKUPENDA ni anguko lako mwenyewe, ndo Maana nasema :-


Kwa tafsiri fupi hakuna Mwanaume anamtongoza Mwanamke bila kuwazia NGONO na wakati huo wewe Mwanamke unakuwa na malengo yako juu ya NDOA. Ndo Maana kwa sasa kipengele pekee kwa Mwanamke kubaini HITAJI LA MWANAUME KWAKE ni pindi tu Mwanamke unapoamua kumpa Mwanaume nafasi ya awali KUFAHAMIANA TABIA na si vinginevyo

Wanawake wengi ili aingie uhusiano ni pindi anapokuwa AMERUHUSU UPWEKE kuendesha HISIA zake, Hapo ni rahisi mno kumpa nafasi Mwanaume ya kushiriki nae ki mwili, kitu ambacho ndicho kinawaliza na Kuwapa kuyachukia MAPENZI



Ndoa nyingi zinalevywa na MAHUSIANO FAKE na niweke wazi hili, Kwenye MAHUSIANO iwe Mwanaume ama Mwanamke wote Wana fake kujaribu kuupata ukweli, Wakati huo Kuna watu wanajua kucheza na SAIKOLOJIA za watu kiasi kwamba unakuwa nae huhisi UONGO ila unaamini katika PENZI ambalo anakupatia, na kwa uhalisia PENZI TAMU unalolipata Kwenye UHUSIANO ni tofauti na utakalolipata Kwenye NDOA na ndo maana NDOA nyingi zinayumba kwa mizania ya MAHUSIANO & NDOA

Taswira ya MAHUSIANO isiibebe taswira ya NDOA huko ni kujitaabisha bure



Kwanini nasema hivyo :-


Mwanamke kutamani ndoa kwa IMAGE ya Mahusiano ni ujinga, Ndoa inatazamwa na jambo kuu moja MWANAUME KUWA MHITAJI WA FAMILIA

Kitu ambacho kwa wanaume wa sasa ni NADRA mno, Yaani mpaka umpate wa hitaji la familia kwa DHATI yake bila kushirikishwa na TAMAA YA MAISHA hapo ni rehema ya MUNGU.
Maslahi yametawala akili za wanaume, na chanzo ni wanawake wanao nunua MAPENZI ndo maana watoto wa mjini husema MAPENZI BILA PESA HAYAENDI



Pesa ni kwa ajili ya MATUMIZI na Mwanaume kama hutafuti pesa yako mwenyewe UTATUMIKA SANA KAMA KALAMU YA MSIBANI

Hitimisho:-

Hatuwezi KUYAKWEPA MAPENZI lakini tusikubari kuwa watumwa wake, Hata URAFIKI mzuri kabla ya NGONO ni FARAJA pia, Japo ujiridhishe kwa tabia na matendo ya mtu ndipo uingie MAHUSIANO.