USHINDI WA MAPENZI NI PAMOJA NA KUWA WA KWANZA KUMUACHA MTU MAANA KUACHWA NI UDHAIFU😂😂
Kuna ugonjwa unatembea kwenye mahusiano mengi japo wahusika hawajaujua, leo nataka niwaambia ni ugonjwa gani;-


Mara nyingi MAHUSIANO yanapokosa mvuto kila mtu hutamani kuyaacha ili akaangalie bahati sehemu nyingine, japo hilo sio suruhisho kwa MAHUSIANO ya dunia ya sasa, Unavyolia inaweza kuwa afadhari ya anayelia bila kumuona, Mapenzi hayana vipeuo wala hayanyambuliki

Tatizo kubwa ni;-

Neno NAKUPENDA linatamkwa mdomoni, Na maana ya UPENDO inatajwa NAFSINI je utajuaje kama ni wewe?


Mtu akikupenda kwa MOYO hachoki kukubeba akilini mwake, Kila Mara atatamani japo akuchokoze tu ili mradi ile sauti ya UPENDO isikike kwako

Lakini pia kubakia kwenye MAHUSIANO yanayoumiza ni kuukana MOYO wako, vivyo hivyo kuyaacha MAHUSIANO uliyopo kisa yanaumiza na kuanzisha Mengine ni KUJITAABISHA





Nini kifanyike;-


Kama hujui kwamba DUNIA tuliyopo Sasa ili upate utakacho yakubidi kugharamia basi wewe endelea kujiamini we mzuri una mashape ama we handsome na six pack yako ili siku ukija kushituka WA FUTURE
yako alisubiri akachoka akajitwalia LIWALO NA LIWE nawe unajiuliza UMUOE/UOLEWE na nani





