JIFUNZE KUVUMILIA KATIKA NDOA, KILA SIKU HAIWEZI KUWA MTEREMKO




Ndoa ni taasisi ya ndoto, ndoto kwa maana kuwa ni kitu ambacho watu wengi hukiwaza kwa muda mrefu, tangu wakiwa watoto. Kwa bahati mbaya kwa walio wengi kabla ya kuingia kwenye ndoa huwaza raha na furaha tu.

Hii inatokana na ukweli kuwa tumelelewa katika utamaduni ambao tunaona aibu kuzungumzia magumu na changamoto zetu. Ni watu wachache sana tena wa kiaSi hiki ambao hudiriki kuongea mapungufu na mabaya yaliyopo kwenye ndoa zao.

Hata wazazi wetu mara nyingi tunahisi kuwa hawagombanagi kwakuwa tu hufanya hivyo kwa siri na kuigiza furaha katika macho yetu. Nijambo zuri sana ambalo husaidia pale wanapopatana au kutatua changamoto zao kukwepa aibu.

Lakini hii inatujengea picha kuwa katika ndoa kuna mazuri tu na hakuna changamoto kitu, ambacho si kweli. Tunapoingia kwenye ndoa na kuona kuwa hatukutani na yale tuliyokuwa tukiyawazia tangu utotoni basi tunakata tamaa mapema.

Hii ndiyo sababu suala la talaka siku hizi limekuwa kubwa. Wanandoa wanashindwa kuvumiliana, changamoto kidogo mshaanza kwenda kwa wazazi ndugu na kulalamika kwa marafiki.

Changamoto kidogo mtu anaanza kukusanya vitu vyake au kuonyesha dharau kwa mwenza wake. Kila ndoa ina changamoto hata hao rafiki zako ambao kila siku unawaangalia na kutamani kuwa kama wao wana changamoto zao wanazokumbana nazo katika ndoa zao.

Tofauti yao na wewe nikuwa tu wao wamejifunza kuongea mazuri ya ndoa zao na kusitiriana mapungufu yao tofauti na wewe ambaye wanajua hata kitandani hamridhishani.

Usidhani wanakuonea huruma unapoongea mapungufu ya mke au mume wako, usidhani kama wanapenda kusikiliza matatizo yako tu, wanakuvumilia kwakuwa tu ni rafiki yao na kwakuwa nao umbea umewajaa.

Wanafurahia kuwa kumbe si wao tu wenye matatizo bali hata wengine wanayo. Jifunze kuvumilia na kabla hujakubali ndoa yako kuvunjika hakikisha umejaribu kila kitu katika kutatua changamoto zenu ikashindikana.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA