MWANAMKE UTAJUAJE KUWA WEWE NI KISIRANI NA UNAMLAZIMISHA JAMAA KUCHEPUKA!
idd makengo
Kuna wanaume wanachepuka kwa umalaya, wapo wengi kama ilivyo kwa wanawake na kuna wanawake wanawalazimsiha wanaume zao kuchepuka hata kama walikua hawana mpango huo. Hata kama mwanaume alishachoka kufanya huo ujinga lakini kuna tabia ambazo humfanya kumchoka mke na hata kumlazimisha kuchepuka.
(1) Kila mume akichelewa kurudia u kupokea simu basi alikua na wanawake zake; Hii inachosha, inawezekana ulimfumania mume wako mara moja, au hata hujawahi kumfumania lakini una visirani vyako kichwani basi kila dakika akichelewa au kutokupokea simu malalamiko ni “Ulikua na wanawake zako!
Hupokei simu zangu, hujibu SMS zangu ulikua unachart na wanawake zako! Unamuona online kama hajakutafuta wewe absi malalamiko ni ulikua na wanawake zako! Kama kila siku hii ndiyo kauli yako kwa mume wako basi jua kama alikua hachepuki unamlazimisha kuchepuka na kama alikua anachepuka basi hawezi kumuacha mchepuko wake kwani ndiyo pekee atakua anampa amani wewe una Kisirani!
(2) Kuwananga marafiki zake na kuwaletea Gubu; Mwanaume ana marafiki zake, inawezekana wana tabia za ajabu au hata hujui tabia zao lakini unahisi wanamshikia akili mwanaume wako. kila akitaka kutoka nao ni kulalamika, kila akiongea nao unalalamika na kumuambia kabisa kua wao ndiyo wanamharibu.
Haiishii hapo, wakija wkako basi unauna, au akitoka nao basi utapiga simu mara kumi kidogo. Hapa kuna mambo mawili, kwanza ni kama unamuambia mume wako kuwa yeye hana akili za peke yake anaendeshwa na marafiki zake, ni kama unamuambia ana kili za kitoto.
Lakini pili ni kama unawaambia marafiki zake kuwa umemkalia mwanaume hakurupuki mbele yako.sababu zote hizi ni mabya kwani ukishamuambia mwanaume ana akili za kitoto arahisi unamdharau, unataka kumkalia kichwani na ukiwaambia marafiki zake unamuendesha basi watamuambia kakaliwa kichwani na hata kumchochea kuchepuka. Kama una tabia hii acha, una KISIRANI.