MSIKILIZE MPENZI WAKO ANAPOONGEA NA YACHUKULIE KWA UZITO MATATIZO YAKE!






Hakuna kitu ambacho kinakera kama kuongea na mtu ambaye unaona kabisa hakusikilizi. Unamuambia kitu ambacho kwako ni chamuhimu au ni kikubwa lakini yeye hasikilizi au husikiliza kwa dharau.

Katika mapenzi hakikisha mpenzi wako anapoongea, anapokuambia changamoto yake, anapokulalamikia na anapoponyesha kuhitaji mtu wa kumsikiliza unakuwa pale kwaajili yake.

Mahusiano ni ya watu wawili mwanaume na mwanamke, hawa kiuhalisia ni viumbe tofauti kabisa kimahitaji kuanzia vitu ambavyo wanavipenda na vile ambavyo vinawaumiza.

Hili unapaswa kulifahamu kuwa kitu ambacho ni muhimu kwako kwa mpenzi wako kinaweza kisiwe na umuhimu wowote, kinaweza kuwa cha kipuuzi. Hivyo hivyo kitu mabacho kwake kina umuhimu kwako kinaweza kuwa hcakipuuzi.

Kwasababu hiyo basi jifunze kumskiliza na kukipa umuhimu kile anachokizungumza kwani kwake kina umuhimu na kukidharau inaweza kumsukuma kutafuta mtu mwingine wa kumskiliza.

Kwa mfano mwanamke anapoongelea viatu au pochi kwa mwanaume inaboa sana kama ambavyo mwanaume anapozungumzia mpira kwa mwanamke. Mjue mwenzako na kuwa bega lake la kwanza la kulilia kila anapokumbana na changamoto ya kimaisha.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA