MWANAMKE KOSA LA KWANZA BAADA YA KUACHWA NA MWANAUME UNAYEMPENDA!
Kuingia kwenye Mahusiano na mwanaume ambaye alikua anakutongoza kabla. Kuna mwanaume alikuana nakutongoza lakini ulimkataa kwakua una mtu wako ukaona atakuharibikia, ukamuambia una mtu wako asikusumbue au hata akamuona mtu wako. Unapoachwa kwakua bado anakusumbua unaona bora niende kuongea na huyu mtu na kurudiana naye.
Hili ni kosa kwasababu kuu mbili, kwanza nikwakua uko kwenye maumivu, akili haijakaa sawa, unaamua labda kwakua umpweke au kwakua unataka kumkomoa X wako, kumuambia kuwa pamoja na kuniacha kuna wengine wananipenda hivyo humkubali mhusika kwakua unampenda bali kwakua ndiyo anakutongoza kwa wakati huo.
Sababu ya pili ni kwakua mwanaume ambaye ulimkataa akajua kuwa umemkataa kwaajili ya mwanaume mwingine ukirudi kwake atajua umerudi kwakua umeachwa, humpendi na huna pakwenda. Kwa kawaida mwanaume huyu hawezi kukukataa, ana hasira za wewe kumuacha hivyo ukimkubali atatembea na wedwe ili kukukomoa.
Hata kama ikitokea akakuoa lakini mara nyingi unakuta anakua na hasira, hajiamini kwakua anahisi humpendi uko kwake kwakua uliachwa.
NINI CHA KUFANYA HAPA; Unapoachana na mpenzi wako jipe muda wa kupona, umia kwanza, lia, ongea na kasirika. Usiingie kwenye mahusiano mengine kabla hujapona, hata kama kuna mwanaume alikua anakutongoza na unamuelewa, umempenda, Basi jipe muda, msahau X wako ili ukiamua kuwa naye uwe naye si kwasababu ya maumivu bali kwakua unamhitaji.
Kuingia kwenye mahusiano harakaharaka ili kumsahau X wako na mtu ambaye ulishamkataa haitakusaidia kwani ma X wana kawaida ya kurudi wakikuona una mtu mpya. Sasa kama hujamsahau na mwanaume anajua ulimkataa kwasababu ya huyo X siku akikuona hata mnasalimiana atajua umerudiana naye na hivyo kuharibu uhusiano wenu.