MWANAMKE ANAPOKUWA NDANI YA PENDO LA KWELI HUWA HANA USALITI WOWOTE

💯
Uonapo Mwanamke kusaliti PENZI ujue mahala alipo ama HAPAMPI FURAHA au HAYUPO HURU.
Maana hitaji kuu la Mwanamke ni UPENDO na ndani ya Mwanaume mwenye UPENDO kuna HURUMA pamoja na UWAJIBIKAJI.
Hakuna dawa ya MAPENZI inayoweza kuroga akili ama moyo wa Mwanamke ila UPENDO❤️
Kama mwanaume hajajua namna ya maana ya andiko;-
👉🏼 ENYI WAUME MUISHI KWA AKILI NA WAKE ZENU.
Ukiambiwa uishi kwa akili na Mke wako haimaanishi etiii UWE NA MFUMO DUME.
Lugha nzuri, masikizano pamoja na kumpa nafasi ya kutoa hoja zake hata kama utazipuuza usionyeshe ila umpe moyo na kumjengea kujiamini ni nguzo kuu ya MWANAMKE KUJIONA ANATHAMINIWA.
Kinachowapa unyonge wanawake wengi ni;-
👉🏼 KUHISI HANA THAMANI.
Ndo maana kumeibuka kundi kubwa na Wanawake kutaka KUMMILIKI MWANAUME na sio kama Mungu alivyomuumba Mwanamke.
Mwanamke wa sasa yupo tayari kupambana kutafuta pesa akijua kwamba WANAUME WA SASA ILI AKUBARI KUWA KWENYE MARIDHIANO LAZIMA MWANAMKE AWE NA PESA.
Na hapo ndipo UPUMBAVU KUTAWALA MAHUSIANO NA NDOA ZA SASA.
Lakini kama Mwanaume atasimama kwenye nafasi yake ipasavyo hakuna Mwanamke mjuaji kwa Mwanaume, Yaani mtu ambaye anajua kwamba AKIWA CHUMBANI ANATAKIWA KULALA MUME AJE JUU anaanzaje kuwa mbabe kwako kama sio wewe ndo unamjengea UJINGA HUO?
Wanaume kuacha MFUMO KANDAMIZI KWA WANAWAKE tukaishi kama vile binti na kijana walivyokua nyumbani njia rahisi kuyasogeza MAPENZI.
Mapenzi ni UPENDO kwa vyovyote vile hakuna namna nyingine kuweza kumfanya mwenza wako AKUTHAMINI na kama thamani yako isipojulikana KWA UJUMLA HAKUNA UPENDO.
Zalisha UPENDO WA DHATI kwa kusimamia mambo haya;-
👉🏼 HURUMA.
👉🏼 UWAJIBIKAJI.
👉🏼 UKARIBU.
Kinyume chake ni ngumu kupata THAMANI KWENYE MOYO WA MTU maana sheria ya MOYO NI UPENDO na kama huwezi kuwa karibu maana yake huwezi kujenga DHAMANA na kama huwezi KUWAJIBIKA tafsiri yake HUWEZI KUSHAWISHI ndipo shida ya wewe kukosa HURUMA itatawala.
Image may contain: 1 person

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA