UNAPOKUWA UNATAFAKARI JUU YA KUFANYA MAAUZI AMBAYO YANAENDA KUGUSA HISIA ZA WATU, BASI CHONDECHONDE USITUMIE HISIA WEWE TUMIA AKILI.


Nafahamu tunajua ila, nataka tu tukumbushane kwenye hili waungana, kwamba matumizi ya hisia zaidi kwenye kufanya maamuzi, yanaenda kuleta matokeo makubwa kwenye hisia za watu hivyo ni muhimu sana kulizingatia hili.
Dunia ilipitia kwenye nyakati ngumu sana miaka ya 1914-1918 na miaka ya 1939-1945, hii ni kwa sababu matumizi ya hisia kufanya maamuzi yalizidi viwango vya akili vya watu fulani walioaminiwa na kufanya maamuzi kwa hatima ya watu wengine.
Nasema tena, kumbuka kwamba kuna maelfu nyuma yako, wataumia sana au watafanikiwa sana kutokana tu na maamuzi utakayo fanya leo.
Leo hii kila mwaka nchi ya Marekani inamlipa Mjapani mamilion ya pesa kwa sababu tu ya mtu mmoja kushindwa kujua kwamba amebeba hatima za watu wengine.
Kuna fursa hutaziona kwenye maisha yako kwa sababu tu ya matumizi zaidi ya hisia kuliko akili
Kuna watu kwenye maisha yako hutafanikiwa kuwaona kwa sababu tu umeshindwa kuzuia hisia zako
Kuna pahala hutafika kwa sababu tu uwezo wa kufikiri na kupata majibu sahihi kwako umekuwa ni mdogo kuliko hisia na tamaa ndani yako.
Jifunze sana kuwa na matumizi sahihi ya hisia.
Ahsante sana.
Msinga

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA