WIVU; NILITONGOZWA KWA NIABA YA MKE WANGU SASA KAONDOKA NA HUYO MWANAUME!

 


Nilikuta meseji imeingia kwenye simu ya mke wangu, ilikua ni Instagra, mke wangu hakujibu. Nilimfuata mke wangu na kumuuliza huyo ni nani, ilikua ni kawaida yangu kufuatilia simu yake na kila mwanaume aliyekua akimtongoza katika mitandao basi nilimfuata inbos na kumuambia aachane na mke wangu.
Ingawa mke wangu alikua hajibu lakini nilikua nakasirika, kuna kipindi alijitoa kabisa katika mitandao ya kijamii ila aakunti zake nikawa nafuatilia mimi. Basi kuna mtu mmoja alimtafuta na kumkumbushia kama walisoma wote, basi nilianza kuchart na huyo mtu bila mke wangu kujua ili kujua kama alishawahi kutembea na mke wangu.
Lakini niligundua kuwa hakuwahi kutembea naye ila alikua anampenda mke wangu na hata nilipomuambia kuwa nimeolewa (nikijifanya mimi ndiyo mke wangu) hakuacha kunitafuta, aliniomba namba ya simu ila niligoma kumpa, basi nikachart naye nikamkubalia ili kutaka kujua kama yuko siriasi au la nilimuambia anitumie nauli.
Katika kutuma nauli nilimpa namba ya mke wangu nikijua kuwa hawezi kutuma. Alimtumia mke wangu laki tano, mke wangu alimpigia simu kumuuliza ni pesa za nini, ndipo naye alishangaa kwani alikua anachart naye kwenye mitandao. Mke wangu alihisi ni mimi kwani ilikua ndiyo tabia yangu, basi alinifuata na kuniuliza na mimi nilimuambia ni mimi ila nilifanya hivyo ili kupima kama wana mahusiano.
Alizirudisha zile pesa akilalamika kuwa nimemdhalilisha, tuligombana kwa muda ila niliomba msamaha, nilitambua kosa langu kuwa nilizidisha wivu basi nikaacha kuchart na huyo mwanaume. Maisha yaliendelea, niliendelea kumfuatilia mke wangu kama anawasiliana na yule mtu au mwanaume mwingine lakini sikuona, nilibaki na amani kidogo kuona kama mke wangu ni mstaarabu.
Lakini miezi sita baada ya lile tukio mke wangu alibadilika sana, kwa kawaida mimi dnito huwa na kisirani, kufuatilia simu zake na alikua anaumie, ila alibadilika, akawa hajali tena, akichelewa tukigombana ananiamboa bora tuachane, nikiongea kdiogo ananiambia kuhusu kuachana, nikimchunguza, nikimpangia kitu hafanyi, yaani akawa yeye ndiyo ana kisirani cha kuachana kuliko mimi.
Zamani nilikua nikimhisi kidogo hata kama si kweli basi namtishia kumaucha, sikua napanga kumuacha kweli ila nilikua namtishia, lakini yeye ndiyo akawa ananitafutia sababu na kuniambia kuwa anataka kuachana na mimi. Basi niliishia kuomba msamaha huku akinikumbushia makosa ya nyumba kuwa nilikua nikimdhalilisha kwa marafiki zake.
Nilikua na tabia ya kushika simu ya mke wangu, kukagua kila jina la mwanaume nampigia kumuuliza kama anamjuaje mke wangu kama ni wapenzi au la ili tu kuona kama anachepuka, basi akawa ananikumbushia na kuniambia kanichoka. Nilishangaa kwani mdua ulikua umepita, tangu kuomba pesa kwa mwanaume mwenzangu na kutumiwa nilaicha hiyo tabia lakini hakujali, alitaka tuachane.
Nilijikuta nachanganyikiwa, napaniki, nakua mtu wa hasira lakini siwezi tena kumpiga kama mwanzo kwani nilikua nahofia ataondoka na mimi bado nilikua nampenda. Haikuchukua muda, aliniambia kuwa hanitaki, alienda kwao kwanza na kuwaambia kashanichoka. Ndugu zake ni kama walifurahia kwani kweli walishanichoka.
Mwanzo nilikua na kawaida ya kila kosa nawaambia wao, nikigombana kidogo nashitaki, nikimpiga wanamuona yeye ndiyo ana matatizo. Ila kuna kipindi walinigheuka na kunichukia kuwa namtesa mtoto wao, nikaacha kuwaambia mambo yangu tena. Alipoondoka na kwena kwao nilijua atarudi lakini alianza mambo ya kudai talaka, niligoma kumpa.
Ila haikuchukau muda, nikajua kaondoka na kwenda kuishi na mwanaume mwingine, yuleyule mwanaume ambaye mimi ndiyo nilimpa namba ya mke wangu. Alikua anatuma mseji kwenye Instagram ya mke wangu mke wangu hamjibu, mimi ndiyo nikamjibu, akanitongoza mimi, nikakubali mimi kama vile anachart na mke wangu, nikampa namba mimi na sasa kaninyang’anya mke wangu.
Nampenda sana mke wangu, sijui hata chakufanya, ni mwaka sasa nimegoma kumpa talaka lakini hajali. Nina watoto wawili na mke wangu, nimewachukua naishi nao lakini mke wangu hajali tena, nimegoma asiwaone ili labda atarudi lakini harusi, sijui kwanini nilifanya hivyo, labda nilizidisha wivu ila nimebadilika na sijui ni namna gani nitamrudisha mke wangu.
MWISHO

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA