Hizi Ndiyo Sababu 4 Zinazopelekea Wanawake Warembo Kutokuolewa

 

 



WANAWAKE Wengi huwa na tabia za kuudhi hali ambayo huwafukuza wanaume walio na uwezo wa kuwaoa
Umewahi kushangaa sababu za wanawake warembo zaidi kutoolewa? Kuna sababu tano ambazo huwafanya wanawake warembo kusalia wapweke.

1. Tabia mbaya.
Wanawake kama hao huwa na tabia mbaya na kuhatarisha nafasi yao ya kupata mume. Wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awe mrembo kiasi gani.

Baadhi ya wanawake hao huwa na maringo sana, eti hawawezi kuosha nyumba kwa kuogopa kucha zao zisikatike. Wengine hawaju kupika na hawawezi kulea watoto kwa kuogopa kuchafuka.

2. Ghali kuwatunza.
Wanawake warembo huwa ghali kuwatunza kwa sababu huwa na dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwa kubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali. Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.

3. Wabinafsi na wenye chuki.
Wanawake wa aina hiyo hufikiria dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanamume. Wanaume wengi hupenda kuhusiana na wanawake wa aina hiyo, ambao huwadharau kutokana na kuwa “wanapendwa” na wanaume wengi.

Wasichojua ni kuwa wanaume huwatumia tu na kuwaacha kutokana na tabia zao ili kutafuta mwanamke mzuri wa kuoa.

4. Hawataki kuwa wazazi.
Wanawake hao hupenda kusalia wakiwa wa kupendeza, hivyo huwa wanaogopa kuzaa wasipate mikunjo, wasinenepe au kuwa na matiti kulegea. Kwa kawaida, hakuna mwanamume anayependa kuoa mwanamke ambaye hawezi kumzalia, hasa kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika.

Kama una sifa za aina hiyo, huenda ni wakati wako kubadilika ikiwa unataka kupata mume.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA