KINACHOLINDA MAHUSIANO NA NDOA NYINGI ZA SASA NI ILE IMANI YA MWANZO NA IMANI HIYO IKITOWEKA NA MUUNGANIKO HUO UNAKUFA

Wengi hawaamini kwamba MWANZO WOWOTE WA MAHUSIANO ni namna gani mtu atapata nafasi, Wengi tunaamini katika kile kilicho tuunganisha na kuwa kwenye UHUSIANO ndipo utakubaliana nami wazi;-


Mwanzo wa Mahusiano na ndoa nyingi watu wanakuwa kwenye USIRI mkubwa, Mtu kuamua kutaka kuwa wazi inaweza kuathiri DHAMANA ILIYOJENGWA KWA USIRI na muda Mwingine mtu kuamua kutaka kuwa mkweli hili nalo linaweza kabisa KUBOMOA DHAMANA ILIYOJENGWA KWA UONGO

Swali najiuliza;-


Hapo nadhani tatizo ni IMANI kwamba mtu anaishi na kile aliamini na kukubari kuwa nawe

Tayari ushadanganywa ila kwa kuwa uko na AMANI Basi ushajizoelea ile hali iliyopo, Muda Mwingine MAHUSIANO AU NDOA inaendeshwa na utulivu uliopo bila kujali ni athari zipi zitakazojitokeza mbele ya safari, Maana kilicho cha muhimu zaidi ni AMANI

Wapo wanaoishi na wenza wao kwa UONGO na wana AMANI kuliko wale wanaoishi kwa UKWELI kwani AMANI ni adimu kwao, Muda Mwingine MAPENZI ILI YALETE AMANI NI MTU KUSIMAMIA UONGO WAKE



Maana unaweza kutaka kuwa mkweli na ukweli wako ukaleta IMANI potofu na kusababisha mporomoko wa AMANI.
Je ni kipi ndicho suruhu ya tatizo la mpasuko wa Mahusiano ama ndoa:-


Ikiwa unaona mtu ameridhika na ulichomuaminisha basi usijaribu kubadilisha, Maana IMANI ndiyo iendeshayo MAPENZI na kama IMANI itatoweka hata uonyeshe UKWELI kiasi gani utaonekana MUONGO TU
