NINI CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MAANA YA UPENDO

Kwanza ifahamike kwamba hitaji la Mwanamke sio hitaji la Mwanaume, Ndo maana wanaume wanalia ki vyao juu ya MAHUSIANO na NDOA zao, na Wanawake wanalia ki vyao kukosa kile wanaamini kinatoka kwa Mwanaume.
Kwa mgongano huo unabaini kwamba;-

Naweza kusema bila woga kabisaa MWANAMKE NDIYE CHANZO CHA MATATIZO MENGI YA MAHUSIANO NA NDOA za sasa,
Ila majibu sahihi ni kwamba Mwanamke alipojikwaa kudai:-



Wanawake wengi badala ya kulilia UPENDO wanahangaika kutafuta ATTENTION ya mwanaume, huku wakisahau kwamba mtu anaweza kabisa AKAKUPA UMAKINI wake ila ndani ya moyo wake haumo, Mwanaume anaweza kukupa muda wake na ndani ya MOYO wake wala hujawahi chungulia, na Muda Mwingine ukapata TENDO LA NDOA kwa wakati sitahiki ila mwenzio anafanya Kama KIBURUDISHO CHAKE wala hutajua



Na ndo maana wanawake mlio wengi mnaangukia mahusiano na ndoa fake kwa kuamini katika mambo mepesi, Mtu hana kazi anakunyimaje Muda wake?
Mtu ana hamu ya ngono unakosaje penzi lake? Mtu anajua anachokihitaji kwako anakunyimaje “ATTENTION” umakini wake

Ukija kushituka UMECHELEWA unaanza kulia na mwenzio alijua yupo kwako kwa sababu zipi, Kitu kigumu kwa Mwanaume ni UPENDO ndo maana wanaume wengi wanafanana tabia zao, Japo naamini kila Mwanaume na hitaji lake kwa Mwanamke, kwamba PAULO anaweza kuwa na HALIMA kwa mtazamo wake, na akiondoka anakuja HAMISI nae atakuwa na HALIMA kwa mtazamo wake japo Mwanamke ni mmoja, Kwa maana hiyo kila Mwanamke ajue wazi :-

Kwamba unapumzika maudhi ya JOHN na kuingia karaha za JUMA

Maana kuachana na Mwanaume na ukapata Mwanaume jikumbushe kwamba SIKU ZOTE PENZI JIPYA LINA RAHA YAKE japo baada ya UPYA ni UCHAKAVU


MTUNZE AKUPENDAYE 
