Kiuhalisia asilimia kubwa ya wanawake wa sasa hawahitaji kupendwa ila wanachohitaji ni kuhudumiwa

...na ni wachache sana wanaofahamu kupendwa ndiyo mapenzi na kuhudumiwa ni jambo lingine tofauti kabisa ingawa lipo kwenye sehemu ya wajibu wa Mwanaume...

Tatizo kubwa lililopo kwa hao wanawake wengi ni kuchanganya vitu viwili ambavyo ni tofauti na kuvifanya kuwa ni kitu kimoja yaani hawatofautishi kati ya "WAJIBU wa Mwanaume" na "UPENDO wa Mwanaume" 
Na ndio maana ni rahisi sana kumsikia Mwanamke leo hii akisema...ikiwa kama Mwanaume hamuhudumii basi huyo mwanaume hampendi, na akihudumiwa kwa fujo ndiyo anajua anapendwa...

Vile vile...

Wanaume wengi wa sasa wao hawapendi kupendwa ndiyo maana wakishajua tu kwamba wanapendwa huwa wanafanya wanavyojisikia...na wale wachache wanaojua thamani ya Upendo ni kubwa kuliko kuwajibika kwao kwa Mwanamke, wao husimamia kwenye Pendo zaidi kuliko huduma...

Shida ni kwamba...

Wale wanaume wachache wanaotafuta Upendo kutoka kwa mwanamke wanakutana na wanawake wengi wanaotafuta kuhudumiwa na mwanaume...

Na wale wanawake wachache wanaotafuta Upendo na upendo kwao ni zaidi ya Kuhudumiwa wanakutana na wanaume wengi wasiohitaji kupendwa.

"...Kabla hujaanza kuyalalamikia Mapenzi...jiulize kwanza Did you choose your partner wisely...?" 
Share

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA