ALIYEONDOKA KWENYE MAHUSIANO AMA NDOA YAKO BAADA YA MIGOGORO HAIMAANISHI HAKUPENDI ILA ANAYEDUMU KWENYE MIGOGORO HUYO NDIYE HAKUPENDI

*
Katika harakati za kuweka sawa MAHUSIANO/NDOA hebu tujifunze hili🤔

Kwanza fahamu kwamba :-
UPENDO WA KWELI HUVUMILIA MABADILIKO.

1 Wakorintho 13:4,6
[4]Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
[6]haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

Huwezi kuwa Kwenye uhusiano ama ndoa ambayo kila ulipojaribu kumsahihisha mwenza wako ndipo hali ilipo kuwa mbaya zaidi, kwamba badala ya kuamini katika MABADILIKO lakini mwenzio ndo kwanza Kosa lile lile ambalo liliwaingiza Kwenye MGOGORO ndilo analolirudia kila Mara, 

Mara nyingi chanzo cha vita za MAHUSIANO AMA NDOA ni Makosa yasiyosahihika, Uvumilivu ambao unatajwa Kwenye MAHUSIANO ni mtu kujua Kosa lake na kujutia, Ila kama bado anakuwa kwenye kukuingiza katika MAUMIVU kwa Kosa ambalo ulimsamehe Mara nyingi MOYO HUWA HAUWEZI KUVUMILIA ikiwa Mtu huyo analo PENDO LA DHATI KWAKO.

Kwanini nikasema mwenye UPENDO WA DHATI ni yule atashindwa kuhimili MIGOGORO na kuondoka ndiye mwenye UPENDO WA KWELI :-

Ukweli ni kwamba "KUBAKIA KWENYE MAUMIVU YA MAHUSIANO NI NGUMU KAMA UNAPENDA KWELI ILA NI RAHISI KUBAKIA IKIWA HUNA UPENDO WA DHATI" kuna mtu huko anađź‘‚ la kusikia au niongeze sauti?

Hivyo usione Mtu ana kuvumilia huku mkiwa Kwenye MIGOGORO isiokwisha ukadhani analo pendo la kweli kwako, Muda mwingine Mtu hana pa kwenda ama ni katika kuangalia zaidi ulichonacho na wengine hata ile hali ya MAZOEA juu yako, Ila ndani yake hana UPENDO JUU YAKO 

Kwa akili zako unagundua kabisa UHUSIANO ama NDOA uliyopo haikupi FURAHA wala AMANI ila unabakia kwa sababu zako tu kisa MTOTO/WATOTO ama MALI unajifahamu kweli
Maana FURAHA NA AMANI ni zaidi ya vitu ndo maana MAHUSIANO yakawa na nguvu kuliko UNDUGU japo ukweli ni kwamba :-
ATAKAYE KUZIKA HUMJUI.

Leo Mwalimu ameamua kuongea🙄🙄

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA