DADA ZANGU KUNA UMRI UKIFIKA UNATAKIWA KUACHA VITU VYA KISICHANA SICHANA


Kuna umri ukishafikia ni lazima kuachana na tabia flani za kijinga jinga na za kiupuuzi puuzi! Kama umefikia umri unasema mimi ni mtu mzima sasa, umeshamaliza shule au chuo, hujaolewa ila una mchumba au mtu wako siriasi lakini kama umeolewa ndiyo haswa, hembu acha mambo ya kuazimana azimana vitu vya kuvaa, kuanzia kiatu, gauni, mawigi, pochi sijui hereni na ujinga ujinga mwingi.

Kwanza acha kuazima na pili usikubali kuazimwa! Mtu anakuazima wigi sijui anakuambia ana mtoko wake, anaenda anavunjwa huko anakurudishia na majanaba yake unakuja tena unavaa mambo yakienda vibaya unamlaumu Mungu kumbe una magundu ya watu! Lakini una mume kabisa anakukuta unachati na shoga yako kuazimana gauni unajua anakuona fala sana, anaona kama kaoa mtoto wa darasa la saba ndiyo anavunja ungo!

Hembu anza kujiheshimu na kuheshimu vitu vyako! Najua umeshaanza kubana pua mimi siazimi rafiki labda mdogo wangu ndiyo tunavaliana! Kuna wakati hata mdogo wako muwe na mipaka! Unamuazima mpaka nguo ya ndani siku akikuazima mume wako utalaumu, ni lazima uanze kujenga heshima katika vitu vidogo vidogo kama mawigi, viatu, nguo kabla ya kujenga heshima katika ndoa yako!

Atamheshimuje mume wako wakati kila akija kwako mnakimbizana chumbani aende kujaribu nguo mpya! Hivi kweli umeolewa mdogo wako chumbani kwako anakuja kufanya nini? Yes najua kuna mazingira mengine ni lazima labda chumba kimoja mnaishi na sebule na wakati mwingine lazima achukue vitu huko ila punguza mazoea! Wanaume si wavungaji akiona unamletea mashoga zako wanamzoea kijinga jinga ipo siku atawachanganya, acha huu ujinga umeshakua mtu mzima yanini kuhangaika na mijasho ya watu!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA