MSICHANA KAMA UNAHITAJI KUWA NA MUME KAMA ALIVYO BABA YAKO UNALO JUKUMU LA WEWE KUWA KAMA ALIVYO MAMA YAKO
Huwezi kukwepa kuwa na mienendo kama ya mama yako kwa baba yako, kwa sababu kila Mwanamke ana wish kuona Mwanaume wake anakuwa kama vile alivyo BABA YAKE MZAZI
Ni nani anayemfanya Baba yako kuwa na mtazamo Mzuri unao uona kwenye ndoa yake na Mama yako kama sio MAMA MWENYEWE
Unajua wanawake wengi hamjui kwamba MWANAUME SIKU ZOTE NI MTU ANAYEHITAJI HURUMA YA MWANAMKE haijalishi ni Mama mzazi, ni shangazi ama dada lakini aliye na nafasi kubwa katika hilo ni MKE
Unapoambiwa;-
HAKUNA MWANAUME MBABE KWA MWANAMKE maana yake ni wewe kujua tabia halisi za mumeo na kujitenga na dharau.
Ndo maana wanawake mliamliwa kuwa na UTII
Hilo pekee ni siraha yako kwenye NDOA yako haijarishi hayo mengine ambayo yatakuwa hayampendezi mumeo, Utii wa Mwanamke umebeba nguvu ya udhaifu wa mwanaume, Ndo maana ndoa za sasa wanawake wengi wanaweka mizania ya BABA NA MUME na kukosoa ndoa zao, Bila kujua kwamba MAMA ndiye aliyefanya BABA kuwa MUME MWENYE HEKIMA NA BABA BORA WA FAMILIA
Anza wewe kuwa kama MAMA yako ili kumfanya Mwanaume awe kama BABA yako ni rahisi sana kuliona PENDO LA BABA YAKO KWENYE NDOA YAKO kwani hakuna Mwanaume anapanga kuharibu NDOA yake ila Mke mwema ndiye huijenga NDOA
Kama unafikiria kuwa na Mwanaume atakayekuwa FALA ili umtawale huku ukijua kabisaa BABA YAKO HAJATAWALIWA NA MAMA YAKO ni kujitukana mwenyewe.
Ijue siri ya MAMA yako kwa BABA yako ili ujue kumfanya Mwanaume wako aendane na hitaji la MOYO WAKO